Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 202
- 167
UTANGULIZI
Tanzania imeendelea kukumbwa na changamoto ya ukatili kwa makundi mbalimbali, watoto wakiwa ni miongoni mwa kundi hili. Kundi hili limekua likikumbwa na adha za ukatili wa jinsi, ndoa, mimba na ajira. Kitakwimu kundi kubwa linaloathiriwa ni la watoto chini ya umri wa miaka 18.
Jamii nyingi zimekua na kasumba ya kuajiri watoto( kazi za ndani/kazibza kilimo na mifugo, biashara ndogo ndogo- shuhuda maeneo ya stendi za magari/mitaani na kuozesha watoto punde wanapomaliza shule za msingi kwa kisingizio kuwa ni kundi lisilo shule tena. Hili limechagizwa na msukumo wa ufuatiliaji wa watoto hawa kuwa mdogo hivyo mwanya kwa ndoa,mimba, ajira na ukatili wa watoto.
Hali ya ufaulu nnchini
Kwa kuzingatia uthibiti wa ubora wa elimu, mitihani imeendelea kutolewa kwa wanafunzi kila wanapotaka kuhama daraja moja kwenda jingine.
Watahiniwa 1,092,960 kati ya 1,356,296 walifaulu katika mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi 2023 likiwa ni ongezeko la asilimia 80.58 ikilinganishwa na ufaulu wa watoto 1,073,402 ya mwaka 2022,( Taarifa ya Matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi 2023,Baraza la Mitihani Tanzania).
Jedwari: Ufaulu wa watoto Elimu ya msingi

Chanzo: Taarifa ya Matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi, Baraza la mitihani la Tanzania, 2023.
Licha ya ufaulu kuongezeka kwa 0.96% hapo juu kuna kundi la watoto wanaoshindwa kufaulu na kuendelea na elimu ya sekondari ya chini. Kundi hili hurudi mtaani na kujihusisha na shughuli zinginezo nnje ya mfumo wa elimu.
Mimba za utotoni,ndoa za utotoni na Ajira za watoto
Vyote hivi kwa pamoja vinaunda "UKATILI KWA WATOTO". Kwa mujibu wa ripoti ya TWAWEZA watoto 3 kati ya 10 waliolewa chini ya miaka 18, idadi kubwa ikiwa kwa watoto waishio vijijini 37% na mjini 21%,(Ndoa za Utotoni Tanzania, TWAWEZA). Kitakwimu mikoa ifuatayo inaongoza kwa mimba za utotoni; Songwe 45%, Ruvuma 37%, Katavi 34%, Mara 31% na Rukwa 30%,( Gazeti la HabariLeo, 28 Octoba,2023).
Hali ya mimba za Utotoni Tanzania.

Chanzo: Taasisi ya TWAWEZA
Hali ya ajira za watoto imeelezwa kuwa ni watoto 3 kati ya 10 wasichana na 1 kati ya 7 wameripotiwa kufanyiwa ukatili kabla ya umri wa miaka 18,(Ukatili dhidi ya watoto Tanzania, Matokeo ya Utafiti wa Kitaifa 2009,UNICEF).
Watoto wengi punde baada ya elimu ya msingi wamekua wakiingizwa katika shughuli za kilimo, ufugaji,kazi za ndani na biashara ndogondogo.
Picha ya Watoto wakichuuza bidhaa mitaani.
Chanzo: mtandao wa Google
Andiko hili litajikita kuangazia watoto walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari ngazi ya chini. Kufuatia uwepo wa kundi hili la watoto ambao huangukia katika changamoto za ajira, mimba, ukatili na ndoa katika umri mdogo.
Ukimya wa sera ya Elimu juu ya kundi la watoto wanaoshindwa kuendelea na mfumo rasmi wa shule ngazi ya sekondari
Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 toleo la 2023 inatambua mfumo rasmi wa elimu kuwa na muundo ufuatao: elimu awali,elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu/ elimu ya amali. Sera imefumba macho juu ya suala la watoto wa darasa la sita watakaoshindwa mitihani ya kujiunga na sekondari.
Uachajwi wa kundi hili unachagiza kwa kiasi kikubwa kutumbukia katika ajira za utotoni, mimba, ndoa na ukatili kwa ujumla. Elimu ya amali sanifu inaingia kwa watoto punde wanapomaliza kidato cha nne, watoto wengi katika kundi hilo huwa wameshavuka umri hatarishi zaidi wa unyanyasajwi( miaka 18). Mfumo pendekezwa wa muundo wa elimu ni 1+6+4+2/3+3, mtoto akipendekezwa kuanza na umri wa miaka 5,(Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 toleo la 2023, Ukurasa wa 36 na 37 kifungu 3.1.1.4 na kifungu 3.1.1.7).
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo haina budi kuja na utatuzi wa changamoto hii. Moja wapo ya suruhu ni mabadiriko madogo ya kisera (muundo) kutazama kundi la watoto hawa.
Mabadiriko ya kimuundo ya mfumo wa elimu
Muundo wa Elimu ujumuishe elimu mbadala kwa watoto wanaotoka katika mfumo rasmi wa elimu baada ya shule ya msingi. Elimu mbadala hii ilenge kundi la wanaoshindwa kuendelea na sekondari( kidato cha kwanza hadi nne). Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Elimu kuingiza kundi la watoto wanaoshindwa mitihani ya Elimu ya msingi. Ili kufanikisha haya serikali ifanye yafuatayo:
- Ifanye utambuzi kila mwaka ya wahitimu wa shule ya msingi wanaoshindwa kufaulu na kuendelea na sekondari.
- Elimu mbadala ianzishwe kwa kundi hili.
- Elimu mbadala ijumuishwe kwenye muundo wa Elimu na kufanywa kuwa ni elimu ya lazima ili kuwalinda watoto mpaka wafikishe umri wa miaka 18.
- Muundo wa elimu mbadala uwe wa miaka 2/3 kikubwa ikilenga kutoa elimu ya ujuzi kwa kundi la watoto hawa. Elimu ya ujuzi iendane na mazingira ya mtoto. Elimu kama ujasiliamali, ufundi,ufugaji, kilimo na fani zinginezo vitolewe kwa kuzingatia mazingira ya mtoto.
- Watoto waandikishwe katika vituo vya mafunzo kwa kuzingatia matamanio yao.
Utekelezaji wa Elimu mbadala
Serikali( Wizara ya Elimu na Mafunzo) kwa kushirikiana na halmashauri husika pamoja na wadau wengine wa maendeleo watafanya uratibu wa mafunzo, ujenzi wa vituo vya mafunzo, utambuzi watoto, ufuatiliaji na usimamizi kwa ujumla.
Nafasi ya wazazi na walezi wa watoto katika kufanikisha zoezi
• Wadau hawa washirikishwe kila hatua ili kufanikisha ufanisi wa mafunzo.
• Wachangie gharama kidogo( kwa wenye uwezo) kwa kukubaliana na vituo vya mafunzo. Hili lisiwe kigezo rasmi cha mtoto kujiunga na masomo. Kwa wazazi watakaowiwa wachangie kwa wasio na uwezo wa kugharamia mafunzo wasilazimishwe.
• Kwa kaya zisizojiweza watoto wapewe ujuzi kwa mkopo, watalipia gharama punde watakapoanza uzalishaji baada ya masomo.
Angalizo: Msingi wa Elimu mbadala uwe ni Elimu bure, mapendekezo hayo juu ni pale tu itakaporazimu utolewaji wa elimu kuwa wa kulipia.
Baada ya mafunzo ya Elimu mbadala
- Halmashauri kuwa na maeneo ya karakana na vituo binafsi vya uzalishaji mali. Watoto( watakaotaka) baada ya kuhitimu mafunzo waingizwe katika shughuli za uzalishaji katika halmashauri ama watu binafsi.
- Wahitimu wapatiwe vyeti vitakavyo wawezesha kujiunga na vyuo vya kati.
- Mikopo midogomidogo itolewe kwa wahitimu na wasimamiwe na wataalamu katika halmashauri kwa uzalishaji wenye tija.
- Vipaumbele na tenda katika ajira zitolewe kwa vikundi katika halmashauri husika.
Faida za utolewaji wa Elimu mbadala kwa watoto watakaoshindwa kuendelea na sekondari ngazi ya chini
• Kupunguza visa vya unyanyasaji, ajira za utotoni na ukatili. Kundi la hili litaingizwa katika mfumo wa ajira rasmi likiwa limeshavuka umri wa miaka 18.
• Kulinda maadili katika jamii, watoto wataendelea kuwa chini ya usimamizi wa mfumo wa elimu mpaka watakapohitimu. Mtoto wa shule huogopwa zaidi kuliko alieko mtaani na hasomi kufanyiwa ukatili japo visa vipo ila kundi hili lina nafuu.
• Kutengeneza uchumi kwa kundi hili na kuinua uchumi wa familia.
HITIMISHO
Elimu ni ufunguo wa maisha na elimu ni dira, shime kwa serikali kubadiri sera yake na kuingiza kundi la watoto wanaoshindwa kufaulu katika hatua za awali ili kulinda kundi hili. Hii ndio Tanzania tuitakayo kwa maendeleo enderevubpasi na utengwaji la kundi la watu katika jamii, muundo wetu wa elimu uwe 1+6+4/3+2/3+3 yaani mwaka 1 elimu awali, 6 elimu msingi, 4 sekondari/3 elimu mbadala, 2 sekondari( kidato cha tano na sita)/ 3 elimu amali na 3 elimu ya juu.
Upvote
2