Mafunzo ya JKT kwa vijana: Ufuatiliaji na Tathmini inahitajika

Mto

Senior Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
170
Reaction score
91
Ufuatiliaji na Tathmini ya Mafunzo ya JKT kwa vijana wanaohitimu Kidato cha sita

Ikiwa ni takribani miaka 3 tangu kurudishwa kwa mafunzo ya JKT kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita, ni wakati mwafaka sasa kama Taifa tufanye tathmini ya kina (Monitoring and evaluation) ya Mafunzo haya kwa kutumia sample ya vijana waliokwisha hudhuria mafunzo hayo na wale ambao hawajahudhuria ili kuelewa kama malengo ya kuanzishwa kwa mafunzo haya yanaekelea kufanikiwa au la, changamoto zilizopo katika kuyaendesha mafunzo haya na maeneo yanayohitaji maboresho.

Ili hiyo tathmini iweze kufanyika kisayansi na kuwa objective ni muhimu sana haya maswali yakapata majibu ya kiutafiti na si kihisia.

- Je lengo kuu na malengo mahususi (main objective and specific objectives) ya kuanzishwa kwa mafunzo haya ya JKT ni yapi hasa?

-Je ni kwa vipi mafunzo na kazi wanazopewa vijana hawa wawapo kambini huko JKT yamelenga katika kuwafanya vijana na Taifa kuyafikia hayo malengo ya kuanzishwa kwa mafunzo hayo?

- Je viashiria/vigezo vya kutathmini (objective indicators for evaluation) vilivyowekwa (kama vipo) kupima kama vijana waliomaliza mafunzo ya JKT wametimiza malengo mahususi ya mafunzo hayo ni vipi?

- Je, ni kwa kiasi gani vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT wamefikia malengo ya kuanzishwa kwake kwa kutumia vigezo vya kupima ufanisi/mafanikio ya mafunzo haya?

- Je kuna tofauti yoyote (a significant difference) kwa kutumia vishiria vya malengo mahususi ya mafunzo ya JKT kati ya vijana waliohudhuria mafunzo hayo na wale ambao hawajahudhuria?

- Ni maeneo gani yanahitaji maboresho au marekebisho katika kuendesha mafunzo ya JKT kwa vijana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…