Mtu Poa 2013
Senior Member
- Mar 26, 2013
- 105
- 65
Hiyo gharama ni 500,000 au?naona ipo chini sana kaka.fafanua zaidi ni material gani zinatumika!
mkuu tunashukuru lakini !!!! angalizo
mafunzo yanayokuwa na mafanikio huendana na vitendo (practical) haswa katika field za kilimo na mifugo .... hivyo ni muhimu tukishuhudia shamba darasa ambalo ni lako wewe na tujihakikishie umewahi wewe mwenyewe kufanya kilimo kwa kutumia greenhouse .... somo la shamba darasa kwa uhalisia litoe mwanga wa gharama zote na mafanikio ya mavuno (yield) hivyo basi hicho kitabu unachouza kitakuwa ni elekezi tu pale unapokuwa unafanya kilimo kwa kutumia greenhouse kwa vitendo
utawahamasisha watu pale watakapoona shamba lako na mavuno yake wewe mwenyewe na siyo shamba la mjomba wako na mamaNa au GreenHouse ambaye ni member humu jf na anayo post ya greenhouse pia alikuwa na kipindi chake katika runinga kituo cha TBC1
vinginevyo mimi naona hii project yako haina tofauti na ku-google ... "greenhouse training manual"
naomba mrejesho
Hiyo gharama ni 500,000 au?naona ipo chini sana kaka.fafanua zaidi ni material gani zinatumika!
Katika nchi hii kla mtu yuko huru kununua au kufanya chochote anachotaka, halazimishwi mtu. Atakayetaka kununua kitabu changu, anakaribishwa. Anayependa vya bure, sawa. Ikumbukwe vya bure huja na strings attached.
Ukisoma uzi huu https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/608513-jenga-greenhouse-kwa-gharama-nafuu.html huna sababu ya kuuziwa material yoyote.
NB: Uliyemuona TBC1 ndiye mimi. Uko huru kuuliza chochote bure.
Katika uzi huo, minimum capital anayohitajika kuwa nayo mtu ni sh mil. 2.5. Nani katika nchi hii mwananchi wa kawaida anaweza kuwa na sh. mil. 2.5? Au na wewe ni capuitalist unavutia biashara kwako? Wale walee

We huwezi tu kuwa na confidence namna hii. Inawezekana aidha watu wananunua sana vitabu vyako maana naona kila kwenye thread zako kuna sentensi ya namna hii. Au umeridhika na maisha. Zaidi nahisi ni kuwa watu wananunua sana copy zako maana kwa ninavyojua watu wengi wanarespond sana katika products zinazohusiana na information.
Kigezo chako kikiwa kipi hasa?
Katika nchi hii kla mtu yuko huru kununua au kufanya chochote anachotaka, halazimishwi mtu. Atakayetaka kununua kitabu changu, anakaribishwa. Anayependa vya bure, sawa. Ikumbukwe vya bure huja na strings attached.
Mkuu, wewe unataka Mtaji wa Mradi wa Kilimo kwa Greenhouse uwe wa Sh. ngapi? Sh. 2.5m bado ni nafuu sana. Jaribu kucheki na Balton (Sijui kama nimepatia Spelling) au cheki na Wakenya kisha ulinganishe bei na hii ya huyu unayetaka kumuita "capuitalist".
Isitoshe huyu Mwananchi unayemwita wa kawaida ambaye hawezi kuwa na Mtaji wa Sh. 2.5m za kuwekeza kwenye Kilimo chenye Tija, ni huyo huyo ambaye ukimpigia hesabu ya fedha anayotumia kunywa pombe na kustarehe kwa Mwaka zinazidi hiyo Sh. 2.5m
Huyo huyo Mwananchi unayemwita wa kawaida anashauriwa aungane na Wananchi wengine ili waunganishe Mitaji na kuweza kuanzisha Miradi ya kuwakomboa!
Nadiliki kusema wewe ni Tapeli ,ulikuja hapa na uzi wako wa kuuza mashine za kutengeneza mkaa,ukarudi na uzi wa kuuza kitabu cha jinsi ta kutengeneza mkaa ,ulipoulizwa maswali ya msingi ukawa unalazimisha watu wanunue kitabu chako.Leo tena unajifanya mjasiriamali wa Greenhouse halafu ukiulizwa maswali ya msingi unaleta majibu ya juuri.