Mafunzo ya Ualimu ngazi ya stashahada ya ualimu elimu ya awali, msingi na sekondari mwaka wa masomo 2020/2021

Mafunzo ya Ualimu ngazi ya stashahada ya ualimu elimu ya awali, msingi na sekondari mwaka wa masomo 2020/2021

stanluva

Senior Member
Joined
Apr 7, 2009
Posts
153
Reaction score
33
Mfumo wa uombaji wa nafasi za mafunzo ya ualimu katika ngazi ya stashahada umefunguliwa. Kama una ndugu au jamaa mtaarifu ikiwa anavigezo vilivyoanishwa anaweza kutuma maombi. Ili kuweza kuona kozi na sifa zinazohitajika tafadhali soma maelekezo kwa kubonyeza hapa.
===
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha NNE na SITA wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III . Waombaji wa Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari kidato cha I-IV. Aidha kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).

AINA YA MAFUNZO NA SIFA
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo

A. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI
Na.AINA YA MAFUNZOSIFA ZA KUJIUNGAVYUOMUDA WA MAFUNZO
1Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi
  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati,English na Sayansi.
  2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC
Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC
Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC
Mpuguso TC, Singachini TC,
Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC, na Dakawa TC
Miaka 3
2Stashahada ya Ualimu Elimu Maalum
  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati na Sayansi
  2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
Patandi TCMiaka 3
3Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali
  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.
  2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC
Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC
Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC
Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Tarime TC
Miaka 3
4Stashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo
  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya sayansi na hisabati.
  2. Aliyehitimu Kidato cha VI au uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza.
Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC
Miaka 3
5Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium)
  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu somo la English
  2. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.
Dakawa TC, Marangu TC
Miaka 3

B. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI
1Stashahada ya Ualimu Sayansi na HisabatiUfaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili katika masomo ya Tahasusi za Sayansi, Hisabati na TEHAMA kwa kuzingatia Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kama ifuatavyo: Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition , Geography, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science.Mamire TC, Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TCMiaka 2
2Stashahada ya Sayansi ya Jamii, Biashara na LughaUfaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili kwa kuzingatia masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari Kidato cha I-IV. Masomo yanayofundishwa katika shule za Sekondari kidato cha I-IV ni : Kiswahili, English, History, Geography, Civics, Commerce and Book keeping.Bunda TC, Mtwara (K) TC,
Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC, Butimba TC, Tabora TC,
Morogoro TC, Tarime TC, Shinyanga TC,
Miaka 2
3Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za MaoneshoUfaulu wa Kidato cha VI kwa kiwango cha Daraja la I-III na alama zisizopungua ‘Principal Pass’ mbili pamoja na ufaulu wa masomo ya liyoainishwa katika mtihani wa kidato cha IV kwa kila kozi kama ifuatavyo:Butimba TCMiaka 2
(a) Sanaa za Ufundi: masomo ya Fine Arts, Basic Mathematics, Chemistry, History, Physics, English na Civil Engineering.Butimba TCMiaka 2
(b) Sanaa za Maonesho: masomo ya English, Literature in English, Kiswahili, Geography na History.Butimba TCMiaka 2
(c) Muziki: masomo ya ‘Music’ pamoja na masomo ya English, Kiswahili, Physics, Geography, History na Biology.Butimba TCMiaka 2
(d) Elimu kwa Michezo: masomo ya Physical Education and sports, Languages, na Biology.Butimba TC na Mtwara (K)Miaka 2

C. MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (STASHAHADA ELIMU MSINGI NA STASHAHADA ELIMU SEKONDARI)
Na.AINA YA MAFUNZOSIFA ZA KUJIUNGACHUOMUDA WA MAFUNZO
1Stashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) MsingiMwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2)Patandi TCMiaka 2
2Stashahada Elimu Maalum (Mafunzo Kazini) SekondariMwalimu kazini aliyepitia mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Stashahada, Stashahada ya Elimu ya Juu au Shahada mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka 2; na
Aliyefaulu masomo ya Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Sita
Patandi TCMiaka 2

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
  1. Tangazo hili halitawahusu wahitimu wa kidato cha Nne 2019 waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu 2020/2021 kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI . Aidha wahitimu wengine waliohitimu kuanzia 2017 hadi sasa wanaruhusiwa kutuma maombi.
  2. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (TCM , au BOFYA HAPA KUJISAJILI/KUINGIA KWENYE MFUMO WA MAOMBI YA UALIMU)
  3. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika Chuo anachotaka kusoma na Vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
  4. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali watachagua tahasusi hadi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
  5. Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
  6. Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
  7. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
  8. Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz , au BOFYA HAPA KUPATA FOMU) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
  9. Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 10/09/2020.
Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu. Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii 0620-198-019
 
Back
Top Bottom