OR TAMISEMI
Ministry
- Jul 3, 2024
- 20
- 93
Akiwa katika ufunguzi wa mafunzo ya mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu leo Julai 9, 2024 Katibu Mkuu Adolf Ndunguru amesema, Serikali inatarajia kuona mafunzo hayo yanakwenda kutatua changamoto za utofauti wa uelewa na tafsiri ya baadhi ya vifungu vya kanuni kati ya Halmashauri moja na nyingine.
Kukosekana kwa utaratibu maalum wa utambuzi na uundaji wa vikundi vinavyotarajiwa kunufaika na mikopo ilisababisha kuwepo vikundi hewa, usimamizi usioridhisha wa mikopo inayotolewa pamoja na marejesho ambayo ilipelekea kusababisha fedha nyingi za marejesho kutorejeshwa kwa wakati.
Pia amesema kukosekana kwa utaratibu mzuri wa usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli zinazofanywa na vikundi vilivyopewa mikopo, kukosekana kwa utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za mikopo, marejesho, vikundi vilivyosajiliwa na shughuli zinazofanywa na vikundi na mapungufu ya Mfumo wa Kieletroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo ILISABABISHA MIKOPO HII KUTOFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA.