Mafuriko Dar: Kwanini ni sahihi Kilaumiwe Chama cha Mapinduzi

Mafuriko Dar: Kwanini ni sahihi Kilaumiwe Chama cha Mapinduzi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Chama hiki kimekuwepo tangu miaka ya sabini. Enzi hizo huku kwetu msimbazi kulikuwa kumejaa simba na wanyama pori.

Sasa chama kilishindwa nini kuweka Ramani ya jinsi ya kupangwa miji ili kucontrol Maji?

Kilishindwaje wakati hakukua na mpinzani?

Nashangaa zaidi baada ya kuna hats baada ya upinzani maeneo Mapya watu wanaishi kiholela na CCM haina plan yoyote ya kutatua tatizo.

Ni aibu
Kila mwaka mafuriko
Kila mwaka kipindupindu Buguruni kwa Mnyamani mwaka huu korona imekipa likizo kipindupindu.

Naandika kwa uchungu sana maana Licha ya Uwepo wa TMA chini ya Serikali makini ya Mh Magufuli hawakuwa na uwezo wa ku-forecast matukio kama la Jana.

Huku Msimbazi tulikuwa tumepanda mbogamboga zetu matembere, michicha,Chinese cabbage, minafu, figiri,Majani ya maboga yote yameenda na Maji. Sisi tulilima kwa timing tukitegemea TMA ikitoa forecast tuvune fasta. Jana machale yalinicheza nikataka kuvuna mboga zote nilivyochungulia updates za weather nikaona kimya jioni nilikuta Eneo lote kama Miami beach.

Mwezi huu wote hatutakula mboga za Majani hivyo zinaweza kutuathili ubongo hata maamuzi yetu ya 28/10 yakachakachuka.

Tuwe makini, CCM kama mmeshindwa mseme apewe hata Mwingine tuone atatufikisha wapi angalau.
 
Back
Top Bottom