Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #41
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kijamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Milioni 20 ili kuboresha mahitimu ya wananchi waliopatwa na madhara ya kulipukiwa na mabomu Mbagala jijini- Mwandishi Wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia Mfuko wa Jamii, Vodacom Foundation, imekabidhi msaada wa madarasa matatu yenye thamani ya Sh milioni 24 kwa sekondari ya Masquaroda, Hanang, Manyara. Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Geofrey Ngatuni na Mkuu wa Mfuko huo, Mwamvita Makamba, kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo. - Habari Leo, Machi 5, 2009
Kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM imetoa msaada wa chakula kwa watoto yatima, wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 65 ambao utagawiwa kwa vituo 30 vya kutunza watoto yatima na wasiojiweza hapa nchini, katika kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. - Radio One Habari, 16 Disemba, 2008
Ndugu zangu hata hivyo vodacom foundation imekwepo kwa kipindi kirefu kwahiyo wanachokifanya sio cha kushangaa ni vizuri na jf nayo kushirikiana na tpn kuanzisha foundation yao kwa ajili ya kupeleka huduma hizi kwa jamii
Kwenye sikukuu za xmass walichangia vituo mbalimbali vya watoto yatima na kwenye sikukuu nyingi sana huwa wanachangia kutokana na hiyo foundation yao , pia kuna michango mengine sio lazima itangzwe kupitia vyombo vya habari kama wewe unavyotaka iwe - naamini vodacom wanatumia haki na wajibu wao kwa jamii kwasababu hiyo foundation ilikwepo toka kitambo mfano mwanakijiji nikuulize mtu akija kuibuka kusema Uliyoanzisha wewe ni SCAM utaweza kubisha ? unachangisha pesa wewe kama nani ? Kisheria
hebu tuangalia kwa sekunde chache...
Hiyo ni mifano michache tu ya jinsi vodacom imekuwa ikitoa misaada mbalimbali. Hata hivyo hii ni mara ya kwanza (kwa kumbukumbu yangu) kwa vodacom ambayo imekuwa ikidai kuwa inatoa misaada hiyo kama sehemu ya "social responsibility" ya kampuni kuanza kukusanya fedha kutoka kwa wananchi halafu kuzirudisha tena kama sehemu ya misaada!
Kwa maneno mengine, kwa kufanya hivyo vodacom haitagusa faida yake au fedha zake yenyewe kusaidia majanga haya au ya huko mbeleni na badala yake itatumia mtandao wake wa simu kukusanya fedha na baadaye kuzirudisha kama sehemu ya msaada. Unless pia wasema kuwa wanamatch shilingi kwa shilingi ya michango inayotolewa hapo watakuwa kwa kiasi fulani wamenivuta nikubali..
mfano mwanakijiji nikuulize mtu akija kuibuka kusema Uliyoanzisha wewe ni SCAM utaweza kubisha ? unachangisha pesa wewe kama nani ? Kisheria
Angalia scam zote duniani zinavyoendeshwa na jinsi hali hii ilivyo sasa au kuna mkataba wa siri kati ya TPN na JF uliowekwa ambao sisi wanachama hatujui ambao unaelezea kidogo kuhusu juhudi hizi za kuchangia waathirika wa mafuriko ? Jamani tusiongelee vitu juu juu tu haya mambo ukianza kuhoji na kufuatilia watu watakimbiana humu
Watu wamechukizwa sana na kitendo hiki kwa kuona kuwa Vodacom inajaribu kwa kutumia nguvu yake kusabotage juhudi za kuchangia Red Cross Society ya Tanzania. Tumeona watu wakijiunga kwenye kampeni yetu kwa sababu sasa wanaalewa. By the way, mafuriko mengine kongwa yamesababisha watu zaidi 300 kukosa malazi. Guess what? Wanasubiri Chama cha Msalaba Mwekundu kuwasaidia...
kwa trend hii muda si mrefu tutasikia barrick na geita pia wanahitaji michango kusaidia kumalizia shule walizokuwa wakizijenga...............
Mimi bado nauliza, Ikwapi serikali kwenye yote haya?
utasubiri hadi kiyama; hakuna serikali duniani ambayo ina rekodi nzuri ya kushughulika na majanga, hakuna. Ndio maana tunatumia taasisi za misaada ya kibinadamu kwa sababu zinaongozwa na vitu tofauti na maadili tofauti. Unafikiri kama Haiti wangekuwa wanasubiri hadi serikali ya Marekani ilete meli zake na misaada yake unadhani chakula kingefika lini? kama siyo Red Cross, Unicef na UN ambazo zilifika mapema pale.
Believe me.. when disaster strike don't count on the government.. waulize New Orleans!
utasubiri hadi kiyama; hakuna serikali duniani ambayo ina rekodi nzuri ya kushughulika na majanga, hakuna. Ndio maana tunatumia taasisi za misaada ya kibinadamu kwa sababu zinaongozwa na vitu tofauti na maadili tofauti. Unafikiri kama Haiti wangekuwa wanasubiri hadi serikali ya Marekani ilete meli zake na misaada yake unadhani chakula kingefika lini? kama siyo Red Cross, Unicef na UN ambazo zilifika mapema pale.
Believe me.. when disaster strike don't count on the government.. waulize New Orleans!
Na hayo madawati yanayotolewa na vodacom foundation pia ni disaster au pia wanafunzi nao watasubiri serikali hadi kiyama