sidhani kama ni Vodacom Alert soma vizuri ni Vodafone Red alert bana. hata nembo ni ya Vodafone kaka. nijuavyo mimi Vodafone foundation kwa kushirikiana na mshirika wake Vodacom Tz (Vodacom Foundation) wame launch hiyo huduma kwa wateja wake waweze kuchangia kupitia sms for the good cause. Vodacom kama kampuni inao uwezo wake wa kuchangia vile vile, hiihuduma inamruhusu mteja yeyote pande zozote za nchi hii kuchangia as little as 250/-. nikiwa kule Musoma na nna only tshs 250/- ntaipeleka wapi? RED CROSS? kuna ofisi pale Musoma? au kule Mpitimbi songea kuna RED CROSS pale? je wataipokea hiyo shs 250/- yangu? hii inakupa fursa mteja wa Vodacom kuchangia popote pale ulipo ktk nchi hii kwa kiwango hicho kidogo. Nijuavyo mimi VODAFONE wameongeza shares zao ktk Vodacom SA, na wao sasa ndio wenye shares kubwa na ndio onwer wa Vodacom SA(South Africa).Outomatically na hii Vodacom ya Bongo inakuwa iko chini ya VODAFONE sasa. Vodafone sasa inajitambulisha katika kusaidia walioathirika na maafa ya mafuriko, kwa kusaidiana na mshirika wake Vodacom TZ, ktk hizo foundations ambako hata VODAFONE ipo, ndio wanakuwezesha na wewe uweze kuchangia waliopatwa na maafa. kama ilivyo ada yetu tumesha jaji kwamba Vodacom badala ya kuchangia wanatuchangisha. lkn wapo watu wanaotaka kuchangia lkn hawajui wapeleke wapi michango yao na hawana mamilioni ya mchango lkn wana vijisenti kidogo km hiyo 250/-. Habari nilizonazo ni kwamba Vodafone alert Tanzania ni ya kwanza kuwa launched ktk nchi zote ambazo Vodafone ina operate. Aim yake ni kusaidia kuchangishana wakati wa majanga kama haya ktk nchi ambazo Vodafone group ipo. Michango bado inaendelea kuchangishwa sijasikia kama imesitishwa, sijasikia au kusoma ni makampuni mangapi tayari yameshachangia yenyewe, sijasikia tamko toka VODACOM kwamba inachangisha TU na haitatoa msaada yenyewe kama kampuni, serikali haijaweka deadline, sisi kama wanachi wa kawaida ni vizuri tukasubiri tuone hii Vodacom inaolaumiwa itafanya nini mwishoni, itatoa pesa yake yenyewe au itachangisha tu. Mwingine alidai ETi VAT ya nini kwenye hizi SMS? sasa hilo suala la VAT ni la ZAKAYO MTOZA USHURU(TRA) na si Vodacom, nijuavyo mie ukifanya biashara lazima ulipe kodi, kwa hiyo hapo VODACOM wanalipa kodi. Mwingine alisema Vodacom kwa nini isipeleke hiyo misaada kwa RED CROSS? kwani wao ndo waratibu wa misaada kwenye majanga mbali mbali, lkn nimeona akina SHYROSE BHANJI wamekwenda mpaka Kilosa (NMB) wakakabidhi misaada kule, kuna wahindi wafanya biashara pale Morogoro, wametoa misaada yao bila kuihusisha hiyo RED CROSS, haikuulizwa kwanini hawakuwasilisha RED CROSS. Anyway Poleni sana wandugu zangu wa kilosa, kuanzia Mbwade, Kimamba, Chanzuru, MADOTO, KILOSA YENYEWE, Ilonga nimeishi huko, mitaa yote naijua kuna secondary flani nilisoma, nakumbuka tukienda Kilosa mjini kuna sehemu mitaa flani ilikuwa ikiitwa DINGILISUSU, tukienda kupata menu pale dah!!! ilikuwa imesimama kinooooooooooooma.