Mafuriko yaizengea nyumba mpya ya Diamond Tegeta

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145

MAFURIKO yanayotokea katika sehemu mbalimbali nchini kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, yanaizengea nyumba ya nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz iliyopo Tegeta Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar. Ukuta uliojengwa baada ya kubomoka. Kwa mujibu wa majirani wa staa huyo, nyumba hiyo imejengwa katika njia ya maji (mkondo), jambo ambalo hakulielewa hapo mwanzo, kwani ndiyo sababu kubwa iliyodondosha ukuta wa uzio wake muda mfupi baada ya Diamond kuhamia wiki kadhaa zilizopita.

Hapa mvua ilipobomoa mara ya kwanza

"Kabla ya ujenzi, kiwanja hiki kilikuwa na njia kuu mbili za maji ambazo wakati wa mvua, zilikuwa zinatiririsha maji kuelekea bondeni, lakini baada ya ujenzi, nguvu ya yale maji yakadondosha ukuta.
"Sasa ukiacha ukuta uliobomoka mwanzoni, kuna njia nyingine ambayo inapitisha maji mengi zaidi ambayo inapita kwenye ukuta wake mwingine na tayari yameanza kuuchimba kwa chini. Mnaweza kuja kuangalia," alisema jirani mmoja aliyekataa kutaja jina lake.
 
Hapo ni ukuta uliojengwa juzi baada ya kubomoka
 
Kwi kwi kwi! Billionaire anajenga kwenye mkondo wa maji? Kwanini asinunue kiwanja sehemu nzuri yenye usalama? Au alipigwa nini?...lol
 
Wangesema kajenga juu mto sawa wacheni mtoto wa watu...

Mbona hawakusema ulipobomoka ukuta mnadhani watoa bima wajinga?

Nyumba ina bima hiyo mwacheni alale...
 
Kwi kwi kwi! Billionaire anajenga kwenye mkondo wa maji? Kwanini asinunue kiwanja sehemu nzuri yenye usalama? Au alipigwa nini?...lol

Ndo mabilionare wetu hao wakibongo angetafta wataalamu waujenzi wampe ramani nzuri au atafte kiwanja sehemu nzuri. Tatizo la Dar watu huwa wanajijengea tu kwakua wana hela. Hapo pembeni nimeona ka mto mvua zikizidi aisee ndo mana ukuta wa mwanzo ulidondoka.
 
Wangesema kajenga juu mto sawa wacheni mtoto wa watu...

Mbona hawakusema ulipobomoka ukuta mnadhani watoa bima wajinga?

Nyumba ina bima hiyo mwacheni alale...

Kwahiyo ni vizuri kujenga nyumba kwenye mkondo wa maji kisa tu una bima? Hahahahahaa.
Kijana kazoea mafuriko kama huko kwao tandale.
 
Kwi kwi kwi! Billionaire anajenga kwenye mkondo wa maji? Kwanini asinunue kiwanja sehemu nzuri yenye usalama? Au alipigwa nini?...lol

Hehehehe

Subiri waje team yake watakuita mchawi

Anyway, labda bilionea anataka kufuga kambale ndio maana akanunua mkondo
 
Hahahahahaa.Halafu eti nae ni mtoto wa mjini jamani ajabu kapigwa kanunua kiwanja kwenye mkondo wa maji!
Ni kweli, nakubaliana na huo ushauri uliompa hapo juu.
 
Hehehehe

Subiri waje team yake watakuita mchawi

Anyway, labda bilionea anataka kufuga kambale ndio maana akanunua mkondo

Waje tu namuogopa nani kwa mfano? Nasema ninachojisikia siogopi watu watachukulia vipi.

Hahahahahaa nijiandae mie kwenda kula kambale boko maana nina ndugu huko.
 
Waje tu namuogopa nani kwa mfano? Nasema ninachojisikia siogopi watu watachukulia vipi.

Hahahahahaa nijiandae mie kwenda kula kambale boko maana nina ndugu huko.

Hahahaah

Bilionea aliona mbali

Kuwa patafaa kwa mradi wa kambale
 
Hahahahahaa.Halafu eti nae ni mtoto wa mjini jamani ajabu kapigwa kanunua kiwanja kwenye mkondo wa maji!
Ni kweli, nakubaliana na huo ushauri uliompa hapo juu.
Tatizo watu huwa hawafanyi tathimini kabla ya kujenga eneo na huyo mtu alijua akauza kiwanja fasta.Hapo ni hatari sana mana maji humfata njia zake za asili ujenzi wa hovyo Dar ni janga sio yeye tu asilimia kubwa ya jiji.
 
Kwi kwi kwi! Billionaire anajenga kwenye mkondo wa maji? Kwanini asinunue kiwanja sehemu nzuri yenye usalama? Au alipigwa nini?...lol

Niliwahi kumshauri aje anunue viwanja bunju beach akusikia sasa kila mwezi wa nne na watano atakuwa anajenga ukuta kama kanoike na janguani, yaani unaweza yanazoa.
 
Tatizo watu huwa hawafanyi tathimini kabla ya kujenga eneo na huyo mtu alijua akauza kiwanja fasta.Hapo ni hatari sana mana maji humfata njia zake za asili ujenzi wa hovyo Dar ni janga sio yeye tu asilimia kubwa ya jiji.

Ni kweli.Sasa yeye kutokana na umaarufu na zile sifa zake hayo atayafuatilia saa ngapi?
Mwisho wa siku kajenga eneo hatari.Mafuriko hayana kipimo, yanaweza kuja mengi hata yakaizoa nyumba kabisa.
Ndio hivyo mtu anajifariji kisa ana bima...kweli?
 
Niliwahi kumshauri aje anunue viwanja bunju beach akusikia sasa kila mwezi wa nne na watano atakuwa anajenga ukuta kama kanoike na janguani, yaani unaweza yanazoa.

Akusikilize wapi yule sifa kibao zimemjaa? Sitoshangaa kusikia kua alishauriwa na wengi pia.
 
Ni kweli.Sasa yeye kutokana na umaarufu na zile sifa zake hayo atayafuatilia saa ngapi?
Mwisho wa siku kajenga eneo hatari.Mafuriko hayana kipimo, yanaweza kuja mengi hata yakaizoa nyumba kabisa.
Ndio hivyo mtu anajifariji kisa ana bima...kweli?

Eneo hilo kila mwezi wa nne wanaamia gest, yeye kajenga ukuta mkubwa akidhani hataamia south africa lakini yakaja wakajitwalia kilicho chake hati!!
 
tuongel;ee wenzetu wa mabondeni huyu ana bima
 
tuongel;ee wenzetu wa mabondeni huyu ana bima
Bima haitolewi kwa watu waliofanya makusudi, hata hivyo inatakiwa ashitakiwe yeye na watu wa ardhi kwa kupima kiwanja kwenye bonde na mataro wa maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…