Mafuriko yaliyokumba Indonesia na Timor Leste yawaua watu 50

Mafuriko yaliyokumba Indonesia na Timor Leste yawaua watu 50

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191

Adonara, East Flores, Indonesia

Flores Mashariki mwa Indonesia ni miiongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo
Watu wapatao 50 wamefariki kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo kukumba Indonesia na Timor Leste siku ya Jumapili.

Mvua kubwa iliyonyesha katika nchi hiyo ilisababisha uharibifu mkubwa huku maji ya mafuriko na mabwawa yaliyojaa yakisomba maelfu ya makazi katika maeneo ya viswani.
Maeneo yaliyoathirika zaidi ni kisiwa cha Flores mashariki mwa Indonesia hadi nchi jirani ya Timor Leste.

Waokoaji wanajaribu kuwatafuta manusura, na maafisa wameonya idadi ya vifo huenda ikaongezeka.
"Wilaya ndogo nne na vijiji saba vimeathiriwa sana," Msemaji wa shirika la Indonesia la kukabiliana na majanga Raditya Jati amewaambia wanahabari.

"Baada ya kuthibitisha data na timu yetu iliyo nyanjani, tulibainisha watu 41wamefariki na wengine 27 bado hawajulikani walipo huku wengine tisa wakiwa wamejeruhiwa."

Hata hivyo naibu mkuu wa Flores mashariki,Agustinus Payong Boli anakadiria kuwa watu karibu 60 wamefariki katika manispaa yake. Idadi hiyo haijathibitishwa na mamlaka nchini Indonesia.
East Flores


Maafisa katika eneo la Flores Mashariki wametoa idadi ya juu zaidi ya vifo japo haijathibitishwa na maafisa wa kitaifa
"55 kati yao, wanatokea kijiji Lemanele," aliliambia shirika la habari la AFP. "Watu wengi walifariki hapa kwasababu walikumbwa na mafuriko na maporomoko ya udongo."
Maafisa nchini Timor Leste wanasema watu wengine 11 walifariki kutokana na mafuriko katika mji mkuu wa Dili.

"Bado tunatafuta maeneo yaliyoathiriwa zaidi na majanga haya," Joaquim Jose Gusmao dos Reis Martins, Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa jamii nchini Timor, aliwaambia wanahabari.

Waliojeruhiwa katika maeneo ya visiwani wameondolewa na kupelekwa vijiji jirani, pamoja na hospitali na vituo vya afya.
Mafuriko na maporomoko ya udongo hutokea mara kwa nchini Indonesia wakati wa msimu wa masika, ambao kawaida huanzia Novemba hadi Machi.
 
Back
Top Bottom