Mekim
New Member
- Mar 30, 2020
- 1
- 0
Katika ripoti nyingi za waandishi wa habari na marejeo ya ripoti ya wizara ya makazi, kila mwaka kumekuwa na ongezeko la idadi ya maeneo kupata athari ya mafuriko kwa mvua za vuli na majira ya dharura (kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa) na yale yaliozoeleka yakiathiriwa kwa wingi zaidi ya awali.
Kila ripoti inapotolewa au maswali ya nyongezwa yakiulizwa bungeni juu ya maboresho ya makazi au fidia kwa watu walioathirika na mafuriko na jitihada za serikali kupunguza atahari hizo, wizara husika imekuwa ikitoa suluhu lisilo la kudumu, pengine halitekelezeki au kujibiwa kwa ajili ya kuridhisha umma, hivyo hili mimi napenda kuita ni mafuriko yasiyo na suluhisho la kudumu, hususani, machoni pa viongozi wetu.
Mikoa ambayo imekuwa ikipata athari kubwa za mafuriko katika majira ya mvua ni jiji la biashara Dar es salaam kwa wilaya zake zote, Jiji la Mwanza kwa baadhi ya wilaya kama Ilemela, Mji mkuu Dodoma, Lindi, Kilimanjaro na mikoa mingine mingi.
Suala la mafuriko na athari zake halijaanza leo au jana, hivyo serikali yetu inauelewa mpana sana juu ya maeneo yanayoqthirikq zaidi na sababu za maeneo hayo kuathiriwa kwa urahisi na mafuriko hata kwa mvua chache kama maeneo ya Jangwani, Tegeta, Posta (kwa Dar es salaam), Msamvu na Dumila ( Barabara ya Morogoro - Dar es salaam - Dodoma) kwa uchache lakini imekuwa haitilii mkazo na umakini katika suluhu ya kupunguza athari hizo, hivyo leo naishauri serikali kuchukua moja kati ya hatua hizi kupunguza au kuondoa mafuriko katika baadhi ya maeneo hususani kati ya makazi ya watu.
KWA JIJI LA DAR ES SALAAM
Ujengwaji wa mitaro
Serikali inapaswa kusimamia na kuhakikisha katika kila eneo linalojaa maji hata kwa mvua ndogo kumewekwa mtaro mpana wenye kuelekeza maji yote baharini, viunganishi vya mitaro viwe na mashimo mapana na ambayo yanaruhusu upitaji wa maji pekee na kuchuja taka zingine, nafahamu mitaro hii ipo katika maeneo mengi ya jiji lakini maeneo kama Posta palipo na ofisi nyingi za serikali hakuna njia hizo za maji, barabara ya Samora AVENUE, nje ya jengo la Air Tanzania, barabara ya kuelekea BARODA bank na NMB bank, barabara ya kati ya jengo la PPF tower na Amana Bank, hay ni baadhi tu ya maeneo ambayo hujaa maji katika kila kipindi cha mvua kwa eneo la Posta Dar es salaam na kusababisha adha na foleni kali kwa wafanyakazi.
Pia kuna maeneo mapya ya makazi ya watu kutoka barabara ya Tegeta kueleke Bunju mpaka Bagamoyo, maeneo haya ni hatari kipindi cha mvua kwani hujaa maji hadi barabarani na hii ni kwasababu hakuna mitaro kabisa maeneo hayo. Mfano kuanzia kituo cha Namanga (Tegeta) mpaka Boko, hizi barabara hujaa maji ambayo hutirirshwa na viwanda vilivyopo karibu na barabara kutoka makazi ya watu, pale tu mvua inapoanza kunyesha, hii husababisha abiria watembea kwa miguu hata kushindwa kufikia combo cha usafiri kituoni au kupanda hata pikipiki kuvuka tu inaongezwa gharama sawa na abiria wa Tegeta kwenda Mwenge.
(Nimeambatisha video juu ya hii hoja)
Serikali iingie mkataba au imagine viwanda hivi kujenga mitaro yao binafsi kwa ajili ya kupitisha maji ya viwanda vyao na isiingile kuharibu miundombinu au kuletq kero kwa mkazi na mpitq njia.
Ubunifu katika kuboresha miundombinu
Kuna baadhi ya maeneo ambayo yanajulikana hata katika ramani ya Taifa kuwa ni maeneo yenye chemichemi za maji kutokana na shughuli zilizofanyika kwa muda mrefu katika ardhi za eneo hilo huko nyuma.
Maeneo haya ni kama Sinza, Survey, Mwenge na Ubungo. Nitazungumzia zaidi eneo la soko lq vinyago Mwenge, pamoja na kuwa na soko la vivutio vya ufinyanzi na tamaduni za kitanzania lakini hili eneo kila mwaka linaripotiwa katika vyombo vya habari juu ya kujaa maji katikati ya uwanja wa soko hili n hata kuingia ndani ya maduka na kusababisha wafanyakazi hao kufunga maduka kwa siku kadhaa.
Eneo la kati ya soko hili linafahamika na kuonekana kuwepo na blonde ambalo ni kivutio kikubwa cha mafuriko hata kwa mvua ndogo.
Wazo langu, katika bonde hili, serikali iwawezeshe wabunifu hao kupata miti au magogo yenye ukubwa usawa wa watu 50 na kuwekwa kati ya lile bonde, wabunifu hao wachonge vinyago katika mti au gogo hizo kila mtu kwa ujuzi wake, vinyago vinachongwa kuelekea juu na kuhakikisha katika maeneo ya pembeni pamebaki eneo dogo kwa ajili ya kupita wateja, pembezoni mwa vinyqgo katika gogo kubwa pawekwe mfano wa mto au mfereji ambao utaruhusu maji kutiririka kutoka kwa vinyago na kuyapeleka moja kwa moja katika mitaro iliyopo pembeni na imefunikwa.
Hii sio tu itaondoa au kupunguza adha ya mafuriko eneo hili lakini pia itaongeza pato kulingana na kivutio hicho.
Kwa maeneo ya sinza na survey na ubungo, haya mengi ni makazi ya watu na wengi walijenga nyumba zao pasipo mpangilio wa kuacha nafasi ya kutosha kwaajili ya mashimo ya choo. Makazi haya mengi huwa na mashimo ya choo mafupi, hivyo mvua inaponyesha mashimo haya hujaa kwa haraka na kurudisha maji nje, wakati mwingine kama nje pamejengewa juu yake basi maji hurudi ndani ya makazi kwa njia ya unyevunyevu na hata kutengeneza ufa kisha chemichemi.
Makazi haya inabidi yaboreshe na pengine kubomoa makazi na kujenga yaliyobora kwa misingi mirefu itakuwa gharama na kuchukua muda, hivyo basi, naishauri wizara ya makazi ifanye ukaguzi bora wa urefu wa mashimo ya vyoo na itolewe kipimo sahihi, kwa wakazi wa nyumba zenye chemichemi za maji, wamiliki walazimishwe kuimarisha ujenzi wa sakafu na kuhakikisha wanaijaza ili kupunguza kasi ya kufikiwa na maji kwa urahisi.
Kwa eneo la jangwani, eneo hili halihitaji kuzolewa michanga (matope) na kuwekwa pembeni, eneo linahitaji ukarabati wa kuipandisha juu barabara, kama serikali ilivyochukua hatua ya kuhamisha wakazi wa eneo lile basi haikupaswa kuweka ofisi kuu ya mabasi ya kwenda haraka eneo lile pia sababu ilishafahamu kwamba ni eneo la kujaa maji kwa mvua za nyakati zote.
Barabara ya jangwani ifungwe kwa miezi miwili, serikali iingie mkataba na mkandarasi wa kuipandisha barabara iwe usawa wa paa la kituo cha mwendokasi, chini kuwekwe mtaro mkubwa wenye kujengewa kwa simenti chini ili kuzuia mchanga kurundikqnq kwa urahisi, ofisi za makao makuu ya mwendokasi ziondolewe eneo lile na zipelekwe eneo kubwa zaidi na lililopo mlimani, nashauri Kimara.
Kwa maeneo ya masoko kama Mabibo na Mbagala, mafuriko ya maeneo kama haya huchangiwa na miundombinu mibovu, upanganaji mbaya wa wafanyabiashara na mlundikano na uchafu katika maeneo ya njia, suluhisho, itapendeza kama masoko hayo makubw ya vyakul yote yakajengwa kwa viwango kama lilivyo soko la kisutu ili kuwepo na mpangilio wa wafanyabiashara na njia ya kutosha kupitisha maji, paa la kuzuia kuingia maji kwa urahisi na hii pia itaziweka salama bidhaa za wafanyabiashara, uchafu ukusanywe na halmashauri kila baada ya siku tatu haijalishi ushuru umetolewa na muuzaji au lah, kama hakulipa mtu mmoja aandikiwe deni lakini sio 500 ya mtu mmoja isababishe athari kwa soko zima na wakati serikali inauwezo wa kusimamia jambo bila hata hiyo 500 kwa muda huo.
Kwa Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza
Mikoa hii huwa inapata athari za mafuriko hasa katika maeneo ya barabara ambazo zimejengwa na kukutanishwq na mkondo wa maji pasipo kuwekewa daraja ili kuipandish qjuu barabara na kupisha njia ya maji, hata hivyo, njia zake za rami bado ni za kiwango cha chini, hata barabara ikijengwa kwa ujazo wa mara tano bado italika pembezoni na kusababisha aidha barabara kupasuka hata kwa mvua ndogo tu na kupoteza mawasiliano kati ya mji mmoja n amwingine.
Katika mikoa hii isiyo na idadi kubwa ya wakazi inabidi miundo mbinu yake itengenezwe kwa kiwango cha juu ili hata ikitokea katika kipindi cha kazi au pikukuu, ambapo idadi ya wakazi imeongezeka basi miundombinu hii iweze kuhimili mabadiliko na kutoruhusu mafuriko kwa haraka.
Tamaa yangu ni kuona waandishi wa habari wakiacha kuripoti habari za mafuriko kila mwaka kama ambayo wanasiasa wanavyopuuzia madhara hayo na maboresho katika majimbo yao na serikali iliyopo madarakani ichukue hatua ndani ya miaka miwili iwe imekamilisha hili, hata tukitoa ripoti za mafuriko ziseme " nchi ya Tanzania imepata mafuriko katika baadhi ya mikoa kutokana na mvua kubwa zinazonyesha na hii ikiwa ni baada ya miaka mitatu bila kupata athari hiyo kwa mvua zote za vuli na masika".
Hii itapendeza, hivyo tunaona hata mafuriko yanasuluhisho la kudumu.

Upvote
2