mafuta ya nazi mamy.
jinsi ya.kuandaa ya kwako mwenyewe
chukua nazi 5 zile ambazo hazijakomaa vizuri amaa ukienda kununua waambie za.mafuta wanazijua zikune utengeneze tui unaweza kuchuja hata mara mbili ili umalize naz yote kwenye mafuta.kisha iweke kwenye chombo kama sufuria hivi liache litulie kea masaa 24/18 nikimaanisha kama umeikuna saa kumi jioni unaliacha usiku mzima mpaka saa nne asubuh ama saa sita mchana utakuta mafuta yamejikusanya kwa juu yaani yametengana na.maji kisha chukua kijiko yachote taratiibu usichote na maji yaweke kwenye sufuria.nyingine kisha chemsha jikoni mpaka yakauke kabisa mradi yasiungue maana mafuta yatakua meusi.ukiona tui lote limeyeyuka bas mafuta utayaona.acha yapoe andaa chombo safi uyahifadhi.kwq hizo nazi 5 unaweza kupata mafuta mil 200 ambayo utatumia kwa miez hata 4 na zaid.
Hakuna mafuta mazuri kwa mtoto mchanga kama ya nazi mamy yana harufu nzuri na yanafaa kwa kurutubisha ngoz ya mtoto pia yanampa mtoto joto la kutosha pia hayana madhara yeyote kwa mtoto hasa uzio.
samahani nimeandika kwa harakaharaka ila naamini utaelewa.