Mafuta gani yatanifaa?

Linamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
9,976
Reaction score
24,496
Wana JF naomba msaada wa ushauri yapi mafuta sahihi kwa ajili ya ngozi yangu,mimi siyo mweusi wala mweupe nipo katikati(maji ya kunde) natafuta mafuta yasiyo cream kwa ajili ya ngozi.Nimetumia NIVEA dry skin na JOHNSON BABY OIL ila bado ngozi siyo nzuri.
 
Je ngozi yako ni ya mafuta au sio ya mafuta?
Kama ni ya mafuta tafuta vipodozi ambavyo havina mafuta.
Hata hizo Nivea nazo kuna ambazo ni kwa ajili ya watu wenye ngozi zenye mafuta na ambazo sio za mafuta. In briefly tafuta lotion au body cream ambazo ni kwa ajili ya 'all type skin'.
 
Ngozi yangu ni kavu,na lotion zote nilizotumia ni za dry skin.
 
Tafuta lotion ya 'vaseline For Men' alafu jaribu kutumia uone itakuwaje.
 
Mkuu.@Linamo Ikishindikana tumia mafuta ya mbadala mafuta ya Zaituni Olive oil ni mazuri kwa mtu mwenye ngozi kavu tumia yatakusaidia hayo mafuta ya Zaituni pia ni dawa ya ngozi kavu.

 
Johnson&johnson lotion ni nzuri sana, unaweza kutumia all skin types ama for dry skin. That is, kama wewe ni mwanaume. Otherwise kuna li-vaseline mafuta flani lina kipicha cha twiga wa njano. Pole sikumbuki brand name yake.
Kwa mwanamke bath&body works ni nzuri zaidi manake ina harufu nzuri za aina mbalimbali.
 
[QUOTE=NEW NOELTafuta lotion ya 'vaseline For Men' alafu jaribu kutumia uone itakuwaje.Haya nilishayatumia bila mafanikio yoyote.
 
Mkuu Linamo Ikishindikana tumia mafuta ya mbadala mafuta ya Zaituni Olive oil ni mazuri kwa mtu mwenye ngozi kavu tumia yatakusaidia hayo mafuta ya Zaituni pia ni dawa.Ahsante nitayatafuta nijaribu nitakupa feedback.
 
Last edited by a moderator:
Johnson&johnson lotion ni nzuri sana, unaweza kutumia all skin types ama for dry skin. That is, kama wewe ni mwanaume. Otherwise kuna li-vaseline mafuta flani lina kipicha cha twiga wa njano. Pole sikumbuki brand name yake.Mi mwanamke,ntayatafuta.
 
Sometimes kula fruits inasaidia kurekebisha ngozi,na maji mengi pia,it helps em jaribu mkuu
 
Mkuu.@ asumpta Haya mafuta huko nyumbani ninafikiri yanauzwa kwenye Ma-Super Market makubwa huku nilipo hatamadukani yanapatikana nipo nje ya nchi huko nyumbani jaribu kwenye hayo Ma-Super Market makubwa yana faida nyingi sana hayo mafuta ya zaituni.

FAIDIKA NA MAFUTA YA ZAITUNI.



Mafuta ya zaituni yana manufaa mengi katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla kama ifuatavyo;


(1)Mafuta ya zaituni hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11 inshaallah.


(2)Mafuta ya zaituni hutibu masheitani kwa kusomea kisomo cha Ruqia, mgonjwa atajipaka mwili mzima mara moja kwa siku pamoja na kutafuna vitunguu saumu punje tatu wakati wa kulala kwa muda wa siku arobaini inshaallah.


(3)Mafuta ya zaituni ni kinga ya masheitani wa kijini na wa kibinadamu kwa kujipaka mwili mzima mara moja kwa siku.


(4)Mafuta ya zaituni hutibu ugonjwa wa mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.


(5)Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.


(6) Mafuta ya zaituni hutumika kama huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au kiharusi hutumia kwa kuchua asubuhi na jioni.


(7) Mafuta ya zaituni hutumika katika kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwanjia ya kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.


(8) Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja.


(9) Tiba ya ugonjwa wa kusahau: paka katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.


(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.


(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa muda wa siku 7 hadi siku 21.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…