BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Ilielezwa kuwa mafuta hayo inasemekana yamenunuliwa katika duka la mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Kamau maarufu kama Mangi ambaye naye alipohojiwa alisema alinunua Tandika.
Baada ya taarifa hiyo mamlaka za Usalama zilitoka na kueleza kuwa watuhumiwa walikamatwa kwa ajili ya hatua za kisheria huku ikielezwa unafanyika uchunguzi wa mafuta hayo kubaini tatizo.
Imepita wiki sasa kupitia vyombo vya habari, Wananchi wamekuwa wakiendelea kudai kwamba bado hawajapatiwa huduma stahiki huku wengine kupitia vyanzo mbalimbali wanadai hata bado hawajafanyiwa vipimo vya aina yoyote na hakuna msisitizo wa tahadhari kuchukuliwa.
Baada ya kusikia na kuona hali hiyo napata mashaka juu ya uwajibikaji wa mamlaka kwenye suala husika ambazo zilitakiwa kubeba suala hilo ambalo linagusa afya za Wananchi wetu, nabakia kujiuliza nini kipo nyuma ya pazia kwa ukimya huo mpaka kushindwa kuchukua hatua za kusaidia waathirika?
Wito wangu kwa mamlaka za Kiserikali kwanza wawasaidie Wananchi walioathirika, pili kuchukua hatua za haraka kubaini na kueleza chanzo cha tatizo hili kuondoa hofu Wananchi wengine kutokana na sintofahamu iliyopo sasa.
Mpaka sasa chanzo rasmi cha tatizo hakijaelezwa ni wiki imepita tunaambiwa uchunguzi unaendelea, tunajiuliza mpaka uchunguzi ukamilike watakuwa wameathirika wangapi?
Nini kinachelewesha uchunguzi kubaini kulikuwepo na changamoto gani kwenye mafuta yanayodaiwa kusababisha changamoto hiyo? Ni vyema tunafahamu ili kama kuna uzembe wahusika wawajibike.
Hili linanikumbusha lile la Wananchi wa Kijiji cha Imalamate, Wilaya ya Busega (Simiyu) ambao waliathiriwa na maji yanayodaiwa kuwa na sumu kutoka katika Mgodi wa Dhahabu wa EMJ, kilichotokea DC akasema Mgodi ulipigwa faini na yale maji yakadhibitiwa lakini walioathirika sijui kama walisaidia.
Sasa swali la kujiuliza Mamlaka za Afya zimeshajua muuzaji wa mwanzo wa mafuta hayo? je mafuta yalikuwa na vitu gani hasa? Hayo mafuta yamesambaa kwa Watu wangapi au maeneo mangapi? Kuna mkakati gani wa kudhibiti Watu wasiendelee kuumia zaidi? Wale walioathirika na hawana hela za kujihudumia wanasaidiwa vipi?