Mafuta ya kupikia ya Alizeti, dumu la lita 20 lafikia sh 120,000/=

Mmea Jr

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
798
Reaction score
1,871
Habari zenu jamani

Bila kupoteza muda ,,, kumeanza kuchangamka, leo hii navyoandika dumu la mafuta ya kupika ya Alizeti huku nilipo limefikia sh 120,000/= ni wiki moja tu nyuma lilikuwa 105,000/=

Ikiwa na maana kwasasa gharama kwa sasa zitakuwa kama ifuatavyo

Lita moja = 6000/=

Nusu 3000/=

Robo. 1500/=

Bei hizi hutofautiaana kwa maeneo au mikoa, mfano mikoa ambayo hawazalishi zao hili la Alizeti bei zinawezakuwa ghali zaidi kutokana na gharama za ziada kama vile usafiri ,, ushuru ambazo hupelekea bei kuwa juu maradafu ukilinganisha na ile wanayozalisha.

Wasiwasi wangu kama mwezi huu wa kumi na moja dumu ni 120,000/= inamaana tutakapo ingia mwezi wa 12, bei inaweza kuwa kubwa zaidi huenda tukanunua dumu la mafuta kwa sh 160,000/= kwa dumu moja hali itakayopelekea gharama za maisha kupanda zaidi hasa katika mwezi huo wenye harakati nyingi za sikukuu.

Ombi

Kama inawezekana serikali ingechukua hatua za haraka kunusuru hali ya ongezo la bei la ghafla linaloikabili bidhaa hii muhimu ,, ikumbukwe mwezi wa mavuto bado mpaka 5 au 6.
 
12K?
120K?

Mkuu mbona Mimi nimenunua hayo mafuta DSM Ila haijafika hiyo bei ya 120K.

Ni juzi hapa
 
Dumu la lita 20 ??

Hapa nazungumzia mafuta ya alizeti
Huku nilipo utaratibu upo hivi

Dumu la lita 20 hupimwa kwa kilo 20 ambapo ukipima kwa lita moja basi utapata lita 21.. wafanya biashara waliokaribu na mashine ( no transportation cost ) wao huu za hiyo lita moja kwa sh 6000/= tu

Na wale waliombali na mashine ( those incurred transportation cost ) hu- charge kuanzia 6500/= na kuendelea

Hivyo kwa upande waKo hebu angalia hayo mafuta uliyonunua ni ya alizeti ?? Isije kuwa umeuziwa maafuta ya kupikia ya safi
 
Habari zenu jamani

Bila kupoteza muda ,,, kumeanza kuchangamka, leo hii navyoandika dumu la mafuta ya kupika ya Alizeti huku nilipo limefikia sh 120,000/= ni wiki moja tu nyuma lilikuwa 105,000/=

Ikiwa na maana kwasasa gharama kwa sasa zitakuwa kama ifuatavyo

Lita moja = 6000/=

Nusu 3000/=

Robo. 1500/=

Bei hizi hutofautiaana kwa maeneo au mikoa, mfano mikoa ambayo hawazalishi zao hili la Alizeti bei zinawezakuwa ghali zaidi kutokana na gharama za ziada kama vile usafiri ,, ushuru ambazo hupelekea bei kuwa juu maradafu ukilinganisha na ile wanayozalisha.

Wasiwasi wangu kama mwezi huu wa kumi na moja dumu ni 120,000/= inamaana tutakapo ingia mwezi wa 12, bei inaweza kuwa kubwa zaidi huenda tukanunua dumu la mafuta kwa sh 160,000/= kwa dumu moja hali itakayopelekea gharama za maisha kupanda zaidi hasa katika mwezi huo wenye harakati nyingi za sikukuu.

Ombi

Kama inawezekana serikali ingechukua hatua za haraka kunusuru hali ya ongezo la bei la ghafla linaloikabili bidhaa hii muhimu ,, ikumbukwe mwezi wa mavuto bado mpaka 5 au 6.
Mitano tena
 
Ndyo mkuu na hapo kuna kila dalili ikapanda zaidi,, wataalamu wa hizi kazi wanasema huenda dumu la lita 20 mwaka huu likafikia 150,000/= kama serikali haitochukua hatua za haraka
Sababu ya yote haya ni nini?
 
Back
Top Bottom