Mafuta ya ubuyu:

cutienoe

Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
38
Reaction score
6
Naomba msaada kwa wataalamu wetu wa afya, hivi ni kweli haya mafuta ya ubuyu yanasaidia kuponyesha ulcers na pia yanasaidia kupunguza weight???? nashindwa kuelewa kwa sababu iweje mafuta yasaidie kupunguza mafuta myenzie mwilini??????Nisaidieni jamani maana nina Ulcers na ni mnene pia.
 
inangeza CD 4... Intibu macho mabovu.. kifupi ni dawa nzuri sana.. ndo maana ina gharama kubwa..
 
Nimeambiwa ni mazuri kwa wazee pia, mwenye kujua yanapatikana wapi anijuze nimpelekee nyanya yangu
 
kwenye saba saba yalikuwepo yalitangazwa sana ila bei tu mtihani
 
Yapo nimeyaona yanauzwa ila bei mpaka naogopa ..its like 100gram package inaenda kam kama 10,000 tshs. Pia nimeona yameandikwa kutibu kama magonjwa 24 bila kusahau yaleeee mambo yetu ya kiume...ndiooo... Nguvuuuuuuu.

Yamenitia wasi kuyanunua maana dose ni vijiko 2 vya chai asubuhi na jioni kwa siku 10 kisha unapumzika 2 weeks then unaendelea kwa style hiyo.

Kwa vile siyajui na weshaingia wajasiriamali niliogopa kununua nisije kununua mafuta ya korie kwa kuchuuzwa ni ya ubuyu kama nilivyonunua oili chafu ilotiwa robo asali nikijua ni asali ya nyuki wadogo.

ni maoni na tahadhari tuu..nothing personel.
 
ivi mtu huwezi kuyatengeneza mwenyewe nyumbani?
ukizingatia mali ghafi inapatikana kiurahisi?
mwenye mbinu atujuze
 
ivi mtu huwezi kuyatengeneza mwenyewe nyumbani?
ukizingatia mali ghafi inapatikana kiurahisi?
mwenye mbinu atujuze

Ni nguvu na muda wako tu. Nenda Kintinku kakusanye ubuyu, utaopata faida mara dufu; kuanzia kwenye matunda, mafuta, na kuni.
 

upo sahihi mkuu
niliuziwa molasses nikaambiwa asili ya nyuki wadogo hii bongo muda sio mrefu watu watauza samli mchanganyiko na wanayojua unaambia mafua ya ubuyu
 
upo sahihi mkuu
niliuziwa molasses nikaambiwa asili ya nyuki wadogo hii bongo muda sio mrefu watu watauza samli mchanganyiko na wanayojua unaambia mafua ya ubuyu
Hahahahaah!! Mimi nimewahi uziwa asali iliyotengenezwa kwa matikiti maji.
 
huwa yanatumika kama kipodozi cha ngozi na nywele worldwide (kwa njia ya kupaka), nilishangaa sana kuona wajasiriamali wa tz wakidai yanatibu magonjwa ya ndani which means mtu anayanywa!
search "baobab oil" ujionee
 
Wakuu mafuta ya ubuyu ni mazuri na ni kweli yanatibu mamdo mengi hasa kuongeza CD4. Ninachopenda kuwatahadharisha watu wameanza kuchakachua ila ukitaka kufahamu ambayo ni sahihi fanya yafuatayo.
1. Rangi yake ni lazima iwe gold light, ukiona ni heavy gold au ni light yellow jua kuna mchanganyo (wanaume clour blind but mnatakiwa kufahamu)
2. Chukua chupa yake halafu inamisha chini na kulaza i.e geuza geuza kila upande, mafuta ya ubuyu huwa hayagandani na chupa hata hivyo hayataonesha mtiririko wowote, ukiona mtiririko jua **** mchanganyo. Kwa wale wanaofahamu Konyagi kawaida ukilaza chupa inakuwa safi kabisa na mafuta ya ubuyu ni lazima yawe hivyo.
3. Mdomoni ni lazima yawe light kabisa, hayana uzito wa mafuta kabisa i.e ni mepeso mno.

4. Taste ya mafuta ya ubuyu ni unique kabisa, ina harufu fulani na ukishaizoea hakuna wa kukubambikiza.
 
Ni kweli yanasaidia kupunguza uzito, sina sababu za kisayansi lakini binafsi nayatumia kwa kunywa mara mbili kwa siku daily, watoto wanapaka katika mwili na nywele. inasemekana yanapunguza maradhi ya kisukari, huwa nanunua k'koo lita Tzs 60,000/= au mtu ananiletea ofisini kwa tZs 40,000/=. K'koo yanapatikana yanapoishia mabasi ya mwenge/tegeta kuna mtu huwa anayauza ukifika hapo yaulizie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…