GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kuna matumaini kuwa huenda mafuta yakagundulika Zanzibar. Ni habari njema!
Hilo likitukia, Tanzania itakuwa tajiri kama Libya ilivyokuwa kabla ya kuangushwa kwa utawala wa Gaddafi?
Sina uhakika kama Gaddafi alikuwa na Maalmasi, Matanzanite, Madhahabu, na Mamikaa ya mawe kama Tanzania, lakini kwa kuwa hayajatusaidia, labda tujaribu kwenye mafuta!
Hata gesi ilipoanza kuchimbwa, kulikuwa na matumaini ya hali kubadilika, lakini ni miaka sasa sisi tulioko huku mikoani hatujui kama bado inachimbwa au la! Hatuuoni utofauti wowote!
Labda, kwa kuwa Maserengeti, Mangororo, na Mamikumi, mabandari na mamito yameshindwa kututajirisha kama mafuta yalivyoitajirisha Libya, tujaribu mafuta!
Tutarajie nini mafuta yatakapoanza kuvunwa Zanzibar? Tanzania itakuwa tajiri?