Mafuta yameshuka bei, EWURA yatangaza bei mpya za April 2023

Mafuta yameshuka bei, EWURA yatangaza bei mpya za April 2023

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi April huku zitakazoanza kutumika Jumatano tarehe 05/04/2023.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mafuta ya Petroli yameshuka bei kwa Tsh 187/Ltr, Dizeli Tsh 284/Ltr na mafuta ya taa 169/Ltr kwa mafuta yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam ikilinganishwa na bei zilizotolewa mwezi Machi.


Screenshot 2023-04-04 at 19.39.41.png
Screenshot 2023-04-04 at 19.40.47.png
Screenshot 2023-04-04 at 19.40.56.png
Screenshot 2023-04-04 at 19.41.03.png
Screenshot 2023-04-04 at 19.41.10.png
Screenshot 2023-04-04 at 19.41.17.png
 
Naona mafuta yanashuka hii mara ya nne sasa, lakini ndugu zangu wa SUMATRA siwaelewi, bei naona ziko vile vile.

Au mimi ndio sielewi [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Italeta ahueni ndivyo unavyoweza kusema, baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo kutangaza bei mpya za ukomo wa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Mabadiliko haya ya bei yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika soko la dunia, gharama za usafirishaji na thamani ya shilingi ikilinganisha na dola ya Marekani.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Aprili 4,2023 na Mkurungenzi Mkuu wa Ewura, Dk James Mwainyekule imeeleza kuwa bei hizo zitaanza kutumika kuanzia Jumatano Aprili 5 mwaka huu.

Amesema kwa Aprili 2023, bei za rejareja za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua petroli Sh187, dizeli Sh284 na mafuta ya taa Sh169 kwa lita ikilinganishwa na toleo la tarehe Machi 2023.

“Kwa mikoa ya Kaskazini Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara, bei za rejareja za Aprili mafuta ya petroli imepungua kwa Sh158, dizeli Sh158 na mafuta ya taa Sh231, ikilinganishwa na toleo la Machi Mosi mwaka huu,” imeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam.
“Bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika,”

Kwa Mikoa ya Kusini Mtwara, Lindi, na Ruvuma, bei za rejareja za Aprili 2023 kwa mafuta ya petroli imepungua kwa Sh220, dizeli Sh220 na mafuta ya taa Sh176 iwa lita ikilinganishwa na toleo la Machi Mosi.

“Kwa kuwa hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika Bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa,”

Katika taatrifa hiyo Dk Mwainyekule alibainisha kuwa tofauti ya bei kutoka sehemu moja kwenda nyingine inatokana na tofauti ya bandari mafuta yanapochukuliwa na gharama ya usafirishaji.

Chanzo: Mwananchi
 
KWA SISI WAPANDA DALADALA ,VYOMBO VYA UMMA WATUSHUSHIE SASA NAULI

ova
 
Shida inakuwaga stolk ya Zamani, alafu bei haishuki kabisa. Ila ikipanda wanapandisha hawasemi stolk ya Zamani. Ewura ni illusion tu.
 
Hakuna kitu
Wanasiasa wangekua hawana percent zao ingeleta maana tunateseka na kodi lukuki yet unaambiwa madarasa na vyoo vimejengwa kwa pesa ya mkopo na ingine ya msaada! Aibu sana
 
Back
Top Bottom