BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 1 Machi 2023. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:- (a Kwa Machi 2023, bei za rejareja za mafuta ya petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam yamepandaa kwa shilingi 149/Lita, shilingi 25/lita na shilingi 37/lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Februari 2023.
(b) Kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), bei za rejareja za Machi 2023 kwa mafuta ya petroli na dizeli yanapungua kwa shilingi 64/Lita na shilingi 209/lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 1 Februari 2023.
Kutokana na kuisha kwa mafuta ya taa kwenye matanki ya kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.
(c) Kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma), bei za rejareja za Machi 2023 kwa mafuta ya petroli zinaongezeka kwa shilingi 138/lita wakati bei ya mafuta ya dizeli zinapungua kwa shilingi 68/lita.
Kwa kuwa hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.
Bei za miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.