Magaidi wanataka nini ili waache hayo mauaji?

Magaidi wanataka nini ili waache hayo mauaji?

superstar1

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2014
Posts
222
Reaction score
176
Jamani naomba mtu mwenye uelewa na hili jambo anieleweshe. Hivi magaidi huwa wanataka nini ili waache mauaji na kutulia? (AlQaeda, Al Shabaab, BokoHaram etc). Kila theory ninayojaribu kuijenga nafika sehemu nakwama. Thanks.
 
Me.nazan.hawa.n.maisha yao hawawez wakaacha...wengine.n.revenge
 
Mchezo huo una mambo wala haufai, Mwenyewe dagaa anataka kuniuzia dagaa naenda sokoni dagaa zinauzwa kila kona
 
Mi naona viongozi wa dini wakutane wajadili madhara ya ugaidi, chanzo chake , Nini nia yao na nani yupo nyuma yao
 
Dunia iwe sehemu salama ya kuishi sasa tukimalizana hivyo tukaishi wapi? Mungu awelegeze na kuwatetemesha ili wakashindwe
 
Kwani umeshawai kujiuliza silaha huwa wanapata wapi? Ukiangalia mipango ya kigaidi huwa inahitaji mipango ya kitaalam na fedha nyingi tu kuifanikisha, nionavo mm nchi zinazotengeneza silaha ndo wafadhili wakubwa wa ugaidi duniani, ukiacha ugaidi uchwara wa rwanda ndani ya kongo" silaha ni biashara kubwa duniani, usipohamasisha watu wapigane utamuuzia nani bunduki na mabimu!?
 
Wana madai yao na yakitekelezwa hayo wasema "wataacha ugaidi" kwa mfano Al shabab watawataka wakenya watoe majeshi yao nchini Somalia na wale Boko Haram wanataka wajitenge na nchi ya Nigeria. Kwahiyo kila kundi linamadai yao japo haijadhibitishwa kweli yakitekelezwa ndio utakuwa mwisho wao.
 
Wakuu binafsi sionagi faida ya vita vya kidini Hususan kipindi hiki ambacho hali ya uchumi ni mbaya mno
 
Jamani naomba mtu mwenye uelewa na hili jambo anieleweshe. Hivi magaidi huwa wanataka nini ili waache mauaji na kutulia? (AlQaeda, Al Shabaab, BokoHaram etc). Kila theory ninayojaribu kuijenga nafika sehemu nakwama. Thanks.
Mtu akizoea kula nyama ya mtu, hawezi kuacha - nyerere
 
Mi naona viongozi wa dini wakutane wajadili madhara ya ugaidi, chanzo chake , Nini nia yao na nani yupo nyuma yao
Sijui kama suala hili ni la viongozi wa dini, gaidi wa kwanza ni serikali ya Marekani, miaka na miaka.
 
Kivipi mkuu?
Hujui watu na viongozi wa nchi mbalimbali waliouawa kwa mgongo wa nguvu za wa Marekani? Mapigano Afrika, ubaguzi wa rangi Afrika ambayo yote yamepelekea mauaji na mateso kwa watu ni ugaidi wao. Yaliyotokea Irak ndio ugaidi wenyewe huo, sasa kiongozi wa dini anahusika aje hapo? Papa John Paulo alimkalisha Bush juu ya Irak na hakumsikia.
 
Unachoongea ni kweli mkuu lakin hakiendan kabisa na definition ya ugaidi
 
Back
Top Bottom