Uchaguzi 2020 Maganja ana hoja zaidi ya Lissu na Magufuli, azawadiwa ng'ombe wawili

Uchaguzi 2020 Maganja ana hoja zaidi ya Lissu na Magufuli, azawadiwa ng'ombe wawili

Alice Gisa

Senior Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
172
Reaction score
417
Maganja hawashinda Magufuli na Lissu mbele ya wafugaji, apewa ng'ombe wawili Mihale, Bunda

Leo tarehe 13.08.2020 nikiwa kijiji kwetu Mihale wilaya Bunda mkoa wa Mara. Nimebahati kuzungumza na Wazee wafugaji nikiwauliza kati ya waliochukua fomu za urais wa Jamhuri ya Muungano. Watu tisa ni nani miongoni mwao salamu zake za kuchukua fomu zimewavutia.

Mmoja wa wazee aitwaye Justine MNANKA akamuita kijana wake na kumuagiza afuate Gazeti la Mwanachi la tarehe 23.09.2019. Kisha akaendelea kwa kusema.

Katika maisha yake mara ya kwanza kununua Gazeti ilikua tarehe 23.09.2019.

Alininua gazeti baada ya kusikia kichwa cha habari radioni kuwa Rais Magufuli ametangaza kufuta mapori 12 na kuondoa mita mia tano za buffer zone kati ya vijiji na hifadhi za taifa.

Na maeneo hayo sasa yatatumika kwa kilimo na ufugaji.

Mzee Mnanka akasema kwa miaka mingi sekta ya ufugaji asilia haijawahi kufikiriwa kitaifa. Matatizo ya malisho na maji yamezaa vifo na hasara za mabilioni kwa familia za wafugaji nchini.

Mzee Mnanka anasema katika watia nia 9 wa Urais ni Bw Maganja Yeremia Kulwa tu ndiye alitamka mwanzo kabisa kuwa anaenda kumaliza tatizo la malisho na maji kwa wafugaji.

Kuwa Bw Maganja mara tu baada ya kuchukua fomu alimuona mubashara Azam Tv akisema atapitia upya mipaka ya hifadhi na kuona nmna ya kupata maeneo ya malisho ya mifugo.

Bw Mnanka anasema kwa tamko hilo anatafuta namba ya simu ya Maganja Yeremia Mgombea Urais kwa tiket ya NCCR Mageuzi. Lengo ni kuchangia Ng'ombe wawili ambao wasaidia fedha za kuendesha kampeni zake aweze kushinda Urais.

Mzee Mnanka anasema Mgombea Tundu Lissu hajui hata kwamba kuna wafugaji nchini. Kuwa Lissu amehutubia makutano zaidi ya kumi tangu achukue fomu ila hajawahi kutamkana neno kilimo au ufugaji. Yeye ni sheria, bunge, Ndege na Risasi.

Anasema Mgombea ambaye ni Rais wa Sasa Dr J. P. Magufuli alijaribu kutatua shida za wafugaji lakini wafugaji hawajaona mabadiliko.
Anasema.

Mnamo tarehe 23.09.2019. Serikali ya awamu ya tano ilitoa Tamko lililoleta faraja kwa wakulima na wafugaji nchini. Tamko lilikua na nia kubwa ya kumaliza jumla jumla kadhia za migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Wafugaji na wahifadhi wa misitu na wanyama. Na kumaliza migogoro yote ya ardhi vijini na maporini nchini.

Tamko hilo lililotolewa na Waziri mkuu wa niaba ya Serikali kwa ujumla lilisema.

SERIKALI YAFUTA MAPORI TENGEFU 12 NA HIFADHI SABA
Kuwa Serikali imeridhia kufuta mapori tengefu 12 yenye ukubwa wa ekari 707,659.94 ambayo yamepoteza sifa na yatumike kwamakazi, kilimo na mifugo kwa vijiji 920.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema Mawaziri wa kisekta wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi walichambua na kuandaa taarifa ya mapendekezo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini iliyowasilishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri.

“Mawaziri walichambua na kubaini kuwa vijiji vyenye migogoro ni 975 na siyo 366 kama ilivyotangazwa awali, Baraza liliamua kwamba vijiji 920 vitabaki ndani ya hifadhi, mipaka irejewe upya, vipatiwe vyeti vya ardhi vya kijiji pamoja na kupangiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Waziri Mkuu alisema Serikali imeridhia Misitu ya Hifadhi saba yenye ukubwa wa ekari 46,715 iliyopoteza sifa itolewe kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za makazi, kilimo na mifugo ili kuwaondolea kero za uhaba wa ardhi.

Na Serikali imeridhia kumega hifadhi za misitu 14 kwa ajili ya kilimo na mifugo na kufuta mashamba 16 yasiyoendelezwa ili yapangiwe matumizi ya kilimo na ufugaji.

Pia alisema Baraza limeamua ardhi ya mita 500 zilizotengwa kama buffer zone (eneo kinga) kwenye maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za wanyama ziachiwe vijiji husika na wananchi wasiondolewe kwenye maeneo hayo.

Akaongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imetakiwa ikamilishe mwongozo utakaobainisha matumizi ya ardhi ndani ya hifadhi ya mita 60 za mito, vyanzo vya maji, maziwa na bahari.

Maamuzi mengine ni kuzitaka Wizara na taasisi zote za Serikali zilinde maeneo yao kwa kuweka alama za kudumu zinazoonekana; na kwamba wananchi hawaruhusiwi kuvamia maeneo mapya na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya uvamizi wowote kuanzia leo.

Anasema Mzee Mnanka kuwa laiti maamuzi haya yangetekelewa kikamilifu na kwa weledi leo dhahama za vita kati ya wafugaji asilia na maafisa wa uhifadhi wa wanyamapori ingekuwa historia.

Lakini kwa kuwa mashine na taasisi za serikali ya awamu ya Magufuli hazikufanyia kazi maelekezo haya. Anaona hii ilikua ni danganya toto tu.

Hivyo Bw Maganja popte ulipo jua wafugaji mkoa wa Mara wako nyuma yako.
 
Ccm bana mwaka huu miti yote inateleza,
Nasikia Kamati kuu mambo yamegoma hesabu zimekataa.
 
Hata kapicha ka hao ng'ombe umeshindwa kuweka ili tuone walivyonona?
 
Huyu Maganja atueleze kwanza je akiingia itahalalishwa au ni jina tu?
 
Back
Top Bottom