Magari aina ya BMW na Mercedez Benz huwa na matatizo gani?

Wanataka prestige wkt uwezo mdogo.

Hata hapa town kuna Bmw 3 series za kawaida tu mtu ameweka badge ya M3,nyingine marcedes za kawaida ila wameiwekea badge ya AMG.

Ndio mambo ya mjini hayo.
 
Haya magari pamoja na Audi mbona engine size kubwa sana?
Unakuta gari ndogo tu size ya IST lakini engine cc 3150

Bmw wana magari yenye engine ya kawaida tu kama 112i,114i,116i,118i,316i,318i,320i,325i,520i,525i na diesel version zake.

Audi zipo pia Audi A3 1.4tfsi,A1 1.2 L TFSI ,A1 1.4 L TFSI etc
 
Mercedes nawaamini sana walitengeneza gari hayana matatizo ya umeme sana kama bmw mercedes ikianza kusumbua ujue imekaa sio bima yenyewe hata toleo jipya inachanganya mafaili...
Mercedes hawakurupukii techs mpya wanaendelea kuboresha zile zile ambazo walishakuwa nazo awali! Kwahio refinement ikifanyika gari inakuwa haisumbui sana.
 
View attachment 443027
Benz ya 2015 model zipo vizuri hizo mashine ni vile kodi yake ipo sawa na bei yake ndio maana tunakimbilia kwenye toyota hiyo gari ugusi kitu zaidi ya kumwaga oil kwa kipindi kirefu sana..
Mkuu,kuhusu haya magari kodi zake,je nikilinunua nje huko mimi mwenyewe nilinunue likiwa used nije nalo hapa Tanzania nitatakiwa kulisajili ndani ya muda gani ?
 
Wanataka prestige wkt uwezo mdogo.

Hata hapa town kuna Bmw 3 series za kawaida tu mtu ameweka badge ya M3,nyingine marcedes za kawaida ila wameiwekea badge ya AMG.

Ndio mambo ya mjini hayo.

M3 au AMG ni engine siyo Badge. Ukilijua hili haikupi shida.
 
Mkuu,kuhusu haya magari kodi zake,je nikilinunua nje huko mimi mwenyewe nilinunue likiwa used nije nalo hapa Tanzania nitatakiwa kulisajili ndani ya muda gani ?
Mkuu gari aina gani unataka wewe ukipenda gari zuri changa tafuta la miaka ya karibuni ulilolipenda nunua tumia mpaka lianze kukusumbua sio leo maana ukiingia humu kila gari ni bovu harafu mtaani hayapo huo ubovu sijui wameujulia wapi...
 
Na ukiingia kwenye Benz hutoki ni gari ya tofauti sana Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…