Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
๐ ๐ฎ๐ด๐ฎ๐ฟ๐ถ ๐บ๐ฎ๐ฝ๐๐ฎ ๐๐ฎ ๐ ๐๐ฒ๐ป๐ฑ๐ผ๐ธ๐ฎ๐๐ถ ๐๐ฎ๐ป๐ฎ๐๐ผ๐๐๐บ๐ถ๐ฎ ๐๐ฎ๐ ๐ธ๐๐๐ฎ๐๐ถ๐น๐ถ ๐ง๐ฎ๐ป๐๐ฎ๐ป๐ถ๐ฎ
Wakati upanuzi wa barabara za Mwendokasi ukiendelea ili kurahisisha Usafiri nchini Tanzania. Tanzania sasa inasubiria mabasi zaidi ya 250 kutoka nchini China ili kuanza kufanya kazi kwa awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka (BRT) yanajulikana kwa jina la "Mwendokasi".
Bado ujenzi unaendelea katika njia mbalimbali zenye urefu wa kilomita 20.3 inayoanzia katikati ya jiji hadi maeneo ya Mbagala kupitia barabara ya kilwa ambayo kwa asilimia kubwa ilikamilika toka Agosti 2024 lakini bado haijaaanza kutumika kutokana na kutokuwepo kwa mabasi hayo.
Mtendaji mkuu wa mabasi yaendayo haraka dar Es salaam (Dary) Bw. Athumani kihamia aliliambia mwananchi kuwa mradi huo wa mabasi awamu ya pili yapo katika hatua ya mwisho ya maandalizi hivyo yanaweza kuwathili kuanzia miezi miwili mpaka mitatu ijayo.
Awamu hii ya pili ya magari yatakua na uwezo wa kutumia Umeme pamoja na Gas magari hayo yanatengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Scania Marcopolo. ambayo lengo ni kuweza kusaidia kwenye kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Gharama zilizotumika kujenga ni dola milioni 159.32 na Kampuni ya Sinohydro Construction limited (SCL) toka China.