Magari mapya yatolewa kwa wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani

Magari mapya yatolewa kwa wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Rais Samia Suluhu Hassann ametoa magari mapya kwa wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Pwani, ili kurahisisha utendaji kazi wa viongozi hao.

Akikabidhi magari hayo kwa niaba ya Rais, mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa magari hayo ili kuwawezesha viongozi hao kwenda kwa urahisi kuwatumikia wananchi vijijini na kuwatatulia kero zao.

Wakuu wa wilaya waliokabidhiwa magari yao leo Desemba 04, 2024 ni mkuu wa Wilaya ya Mafia, Halima Mangosongo, mkuu wa wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Fredrick Komba na mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Saimon.

Hii nia awamu ya pili kwa wakuu wa wilaya za Mkoa wa Pwani kukabidhiwa magari, ambapo awamu ya kwanza wakuu wa wilaya za.Kisarawe na Bagamoyo walikabidhiwa magari mapya, na mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo yeye atakabidhiwa katika awamu ya tatu.​
Screenshot 2024-12-04 170305.png
 
Japan viongozi wanatumia escudos na rav 4, mafukara haya yanaendav kununua mav8! Halafu wajapan wanawachora TU! Miafrika!!!
Kuna ile story ya wajumbe wanaenda Paris club kwenye mkutano wa nchi tajiri kufanya makubaliano ya kusaidia nchi maskini. Kwenye ndege amekaa mjumbe wa nchi tajiri yupo economy class huku mjumbe wa Afrika anayekwenda kusaidiwa yupo first class. Tafakari.
 
Anawakosea sana viongozi wetu watukufu.Angalau ingekuwa chopa au ndege ,kila mmoja yake.
 
Back
Top Bottom