Magari toka China

Dumelang

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
3,204
Reaction score
5,710
Wadau tujadili magari ya mchina naona soko lake hatujalichangamkia lakini hawa jamaa wana gari nzuri sana, zingine kama vipanya tu kuanzia 2500 usd, lakini wana SUVs unapata kwa bei simple tu, nilikiwa nacheki usd 12000 nakuendelea unaweza pata gari 0km

Kwanini hatumwamini mchina wakati kwasasa anaaminika anatupatia mabasi zimejaa yutong na nduguze mitaani, mashine kama Escavator, magari ya mchanga dumper, grader, nk siku hizi zimejaa kwa wakandarasi kulinganisha na CAT na BENZ nk, watu wanatumia mchina kama Lihong, Linglong kwakuwa ni nafuu affordable na easy to mantain

Je ni muda tuanze kujilipua na Sedans, SUV za mchina? Kama ndio kwanini hatujaona hio fursa ya kumiloki michuma?

Raha ya mchina anakupa mwonekano wa gari ya mjapan ya mwaka 2023 ya milioni 500, mchina anakupa mwonekano huohuo na kuzidi kwa milioni 40

Note: Marekani sasa wanazitumia sana gari za mchina.

Karibuni kwa maoni, mjadala na mitazamo

-Dumelang View attachment 2776648View attachment 2776650View attachment 2776655
 
Kweli wana gari nzuri sijui tu ubora wake....
 
Gari za Mjerumani mmezipa kila aina ya matusi, Hizo za mchina mtaziweza?

Nimewahi kukutana na pick truck moja ya mchina, umeme kama wa mjerumani.
 
nadhani ni kwa sababu magari yao mengi ni left hand drive kama ilivyo marekani, tofauti na japan,europe ni right hand kama nchii nyingi africa
 
Kwenye simu, redio, tv sawa ila kwenye Gari.......Usituchee uhai bado tunautaka hata kama ni maskini
 
Ikiwa wakandarasi wa kichina wanatumia toyota hilux na Nissan hardbody kwani hawakuziona izo gari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…