Magari ya dharura ni yapi, na je yanaruhusiwa kuvunja sheria?

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
[Kifungu cha 54 cha Sheria ya Usalama Barabarani]

1. Bila kujali vifungu vya sheria ya Usalama Barabarani na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 54, dereva wa gari la dharura, ikiwa ataona kuwa kuzingatia sheria kutazuia matumizi ya gari la dharura kwa kusudia lililotarajiwa, anaweza kufanya lolote kati ya yafuatayo:

(a) Kuegesha gari mahali popote barabarani bila kujali sehemu hiyo ni maegesho au la

(b) baada ya kupunguza mwendo kadiri itakavyokuwa salama, akaipita alama inayomlazimu kusimama

(c) kuzidisha mwendo kupita ule unaoruhusiwa kwenye barabara hiyo ili mradi tu hahatarishi maisha au mali; au

(d) anaweza kupuuza sheria yoyote inayoongoza muelekeo wa magari au kupinda kwenye muelekeo wowote.

Masharti ya kifungu hiki.

2. Ruhusa iliyotolewa na kifungu hiki kwa magari ya dharura itatumika tu pale ambapo dereva wa gari hilo awapo kwenye mwendo atakuwa anapiga kingóra au filimbi, kadiri inavyowezekana au pale ambapo gari litakuwa na kimulimuli basi atawasha kimulimuli kitakachoonekana wakati wote kwa umbali wa mita 150 toka mbele ya gari.

3. Masharti ya kifungu hiki hayatamuondolea dereva wa gari la dharura wajibu wa kuchukua tahadhari na kuendesha kwa umakini kwaajili ya usalama wa watu au mali, na hakitamlinda dereva kutokana na madhara ya kutoendesha kwa umakini (uzembe) utakaosababisha madhara kwa watu au mali.

4. Kwa minajili ya kifungu hiki magari ya dharura inamaanisha magari ambayo yanatumika mara kwa mara kwa shughuli za polisi, zimamoto, magari ya wagonjwa, magari ya majeshi, na magari mengine ambayo kwa amri ya Waziri iliyochapishwa kwenye gazeti la serikali yatatajwa kuwa ni ya dharura.

Admin 1

RSA Tanzania
Usalama barabarani ni jukumu letu sote
 
Wale jamaa wa geti jeusi mbona sijaona wametajwa hapo, wanatusumbua sana hii barabara ya Mbezi huku na migari yao kuendesha wrong direction, kulazimishwa wapishwe
 
Wale jamaa wa geti jeusi mbona sijaona wametajwa hapo, wanatusumbua sana hii barabara ya Mbezi huku na migari yao kuendesha wrong direction, kulazimishwa wapishwe
Ni maderava nao wanavunja Sheria sema wanalindana
 
Leo nimeona gari ya Jaji yenye plate namba J alafu namba yake ni hamsini na kitu Inapita katika barabara ya mwendokasi kinondoni, sasa nikajiuliza kama Jaji anavunja sheria inafundisha nini raia
 
Leo nimeona gari ya Jaji yenye plate namba J alafu namba yake ni hamsini na kitu Inapita katika barabara ya mwendokasi kinondoni, sasa nikajiuliza kama Jaji anavunja sheria inafundisha nini raia
Ujuzi wa dereva, sema ni hatari sana sema noma hakuna
 
Kwahyo ni sawa tu Jaji ambaye ni mtafsiri na msimsmia sheria mahakamani akiwa anavunja sheria barabarani?
Jaji anadharura gani? Ni matumizi mabaya ya madaraka, na hii ni sifa ya wote walioko serikalini, mfano magari yenye namba za serikali jinsi yanavyokimbizwa na kupita watumiaji wa barabara kwa hali ya hatari.
 
Nilivyoona jaji anavunja sheria nilitaman litokee gari limsombe yule jaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…