Magari ya Kubeba wanafunzi bado yanakaguliwa au hadi ajali itokee?

Magari ya Kubeba wanafunzi bado yanakaguliwa au hadi ajali itokee?

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Imekuwa ni kawaida kabisa uwajibikaji Umekuwa ukifanyika vizuri zaidi pale kitu kinapotokea.

Na mara nyingine taratibu mbali mbali zinaanzishwa ili kuhakikisha tatizo halijirudii tena.

Lakini cha ajabu baada ya muda mambo husahaulika na kutowajibika kunaendelea.

Tuendelee kukumbushana wajibu japo wengi hawapendi kukumbushwa.

Sina uhakika kama Matron wapo kwa magari ya watoto kama ilivyoelekezwa?

Tuendelee kufuatilia hili na kutoa taarifa kwa kuwa watoto ni taifa la Kesho.
 
Uwajibikaji mpaka maafa yatokee ni tatizo sana hapa nchini.
Mbaya zaidi, hata yanapotokea hayo maafa, waliyoyasababisha hulindana
 
Back
Top Bottom