SoC02 Magari ya umeme Tanzania

SoC02 Magari ya umeme Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Fortuworker

Member
Joined
Sep 5, 2022
Posts
10
Reaction score
21
Najua huenda hujaendesha gari la umeme au hata hujawazia kununua gari hilo, Unaambiwa Ufunguo wa Mafanikio Ni kuanza Mapema, kabla ya Muda kufika. Kuna Wakati Sisi hapa Tanzania, Vituo vyote vya Mafuta, Hatuta kuwanavyo Badala yake Tutakuwa na Vituo vya kuchaji.

Tuko katikati ya mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa teknolojia na Mapindunzi ya Kiuchumi, hasa katika utengenezaji wa magari. Tangu Henry Ford alipoanza kutengeza magari ya kwanza mnamo mwaka 1913.

Wadadisi wengi wa tasnia ya utengezaji magari wanaamini tayari tumepata mahali ambapo mauzo ya magari ya umeme yatazidi magari ya petroli na dizeli kwa haraka sana. Bila shaka huenda watengenezaji wakuu wa magari wanatilia wazo hilo maanani.

Ukweli ni kwamba, serikali kote duniani zinaweka azimio la kupiga marufuku uuzaji wa magari yanayoendeshwa kwa petrol na dizeli kutokana na mabadiliko makubwa ya tabia nchi na uchafuzi mkubwa wa Hali ya hewa Duniani. Na kupatia kipaumbele mchakato huo.

Magari ya Umeme ni mapinduzi ya kiteknolojia na uchumi ambayo huwa inatokea haraka sana. Hapa wazo langu ni kwamba, ubunifu, Teknolojia na Ujuzi. huanza polepole, kwa kuwavutia tu. wale wanaopenda mambo mapya.

Tumeona maboresho makubwa ya Kampuni mbalimbali katika Magari yanayoendeshwa kwa nguvu za umeme, Lakini Tajiri Bwana Elon Musk, Amefanikiwa Na Gari la
Tesla Model 3. Na ndio gari ya umeme inayonunuliwa sana Duniani

Tesla Model 3. Ina mabadiliko makubwa ambayo yako kwenye betri na bei. Hii inaashiria mwanzo mpya uliofanya kuwa rahisi kununua magari hayo ukilinganisha na aina nyingine ya magari.

Huku hayo yakijiri , kiwango cha nguvu inayoweza kupakiwa kwenye kila betri - inaendelea kuongezeka. Pia yanadumu kwa muda mrefu. Betri ya kwanza duniani inayoweza kuendesha gari kwa maili milioni ilizinduliwa na mtengenezaji wa betri wa China, CATL.

Tanzania magari haya ya Umeme inaweza kuwa fursa Nzuri Kiuchumi siku za Usoni. Kama Tutaanza Mapema kabla ya Muda, kwasababu gharama yake ni nafuu hasa kwa magari yanayoedeshwa kwa muda mrefu.

Mpango Biashara kwa matumizi ya magari ya umeme Tanzania. kinachohitajika ili hii teknolojia ifanye kazi Ni:-
1- kuanzisha Kampuni ya Usafiri, Kama Uber inayotumia magari ya umeme.
2- Vituo vya kuchaji vitakavyotumia Umeme wa Jua.
3- Betri zenye Nguvu
4- Mafundi wenye ujuzi wa umeme wa magari.
5- Gharama Nafuu ya Uendeshaji.

01. Kuanzisha Kampuni ya Usafiri.

Tanzania Ni Nchi ambayo Inakuwa kiuchumi Kila kukicha, Ongezeko la Watu na Mzunguko Mkubwa wa Shughuli za Kiuchumi nao, unazidi kuwa Mkubwa Kila Siku. Na Nchi hii, ili iendelee kupiga Hatua kwa haraka ndani ya Afrika Mashariki na kusini Mwaafrika. Inaihitaji Miundombinu ya Usafiri inayoenda haraka, rahisi na Nafuu Sana.

Tumeona Juhudi za Serikali kukabiliana Mapema na Matarajio ya mabadiliko Kiuchumi. Kwa kuanza kuanzisha Usafiri wa mabasi ya mwendokasi, ndani ya Jiji la Dar es salaam. Na Ujenzi wa Reli ya kisasa, inayotumia Umeme kutoka Dar es salaam, Hadi Mwanza.

Lakini Sambamba na Hayo. Tumeona Pia, Kampuni za Usafirishaji Abiria Maarufu Kama, Uber. Nazo zikiendelea kupambana kutoa Huduma Mtandao, kwa Abiria wao. Lakini Siku za Hivi karibuni kumekuepo na changamoto kubwa kwa waendeshaji wa hizo Kampuni, Juu ya Uendeshaji wake kulingana na Ongezeko la Bei ya Nishati ya Mafuta.

Njia ya Kuweza kutatua hii Changamoto. Ni kuanza kutumia Magari ya Umeme, Tanzania. uanzishaji wa Kampuni ya magari yanayotumia Umeme. Ndani ya majiji makubwa ya Tanzania Kama. Dar es salaam, Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya. Hii italeta Uhakika. Uhakika huu ambao utawahakikishia watanzania, Ufanisi na Ubora wa Magari haya ya Umeme, kuanza kutumika. Hata kwa Kila Mmoja anaetumia Chombo Cha Moto.

02. Kuanzisha Vituo Vya kuchaji.

Tanzania inakampuni Nyingi sana, zinazojishughulisha na uagizaji na uuzaji wa Nishati ya Mafuta ndani na nje ya Nchi. Nishati ya Mafuta Ni bidhaa ambayo inashikiriwa na uchumi wa nchi tajiri na zenye uwezo Duniani.

Twakwimu za Sasa za Bara la Afrika. Ni bara ambalo ndio linategemea zaidi kutumia Nishati ya Mafuta Katika Juhudi zake za kuendelea kustawisha uchumi wake. hii inaweza kuwa Tamu au Chungu kwa Afrika. Lakini Pale inapotokea Vita ya uchumi au mporomoko wa Bei Katika soko la Dunia.

Nishati ya Mafuta Ni bidhaa inayoagizwa kwa wenzetu, nje ya nchi. inahitajika Gharama kubwa kusafirishwa, kuhifadhiwa. Na mfumo wake wa matumizi Hadi kumfikia Mtumiaji wake Pia inahitaji Gharama kubwa. Vilevile Nishati Hii inaweza ikaleta Athari na Majanga Katika Matumizi na mazingira yetu.

Sasa Uanzishwaji wa Vituo vya kuchaji vyombo vya Moto, Ni kwa kutumia umeme wa kawaida kutoka grid ya Taifa, na umeme wa jua yaan (Solar). Hii itatusaidia kupunguza Gharama. Pia athari Ndogo za mazingira na Majanga Katika Matumizi.

Kwahiyo, vituo hivi Vya kuchaji Magari ya Umeme vitajegwa Kama vilivyo Vituo vya Mafuta, vilivyo vya Sasa. ambavyo vitakuwa na uwezo wa kubadili Nishati ya umeme wa Jua na kuwa umeme wa kawaida. kwakutumia sahani (Solar Panels). zinayokusanya Mwanga na mionzi ya jua. itakayoezekwa juu ya kituo Cha kuchaji Kama bati. Na nguvu Hiyo ya Umeme iliyokusanywa kuhifadhiwa kwenye Betri, Betri zenye Umeme ambazo zitakuwa zinafanya kazi ya kuchaji Magari yaliyo tengenezwa kwa mfumo wa umeme. Yanayohitaji kuongezewa Nishati Hiyo.

Mfumo huu wa kuchaji Magari ya Umeme, haitakuwa tu vituoni, bali hata Nyumbani. Ni kulingana na uwezo wa Gari kupokea kiwango na kiasi cha umeme kinachohitajika. Lakini mfumo wa haraka/Muda mfupi (SuperFast charging) na wa kisasa kabisa kuchaji utapatikana vituoni kwa Bei Rahisi.

03. Uwezo wa Betri zenye Nguvu.

Tanzania Ni Nchi Yenye Miundombinu ya Barabara, ambazo nyingne bado azijatengenezwa, kwa kiwango cha Lami. Hasa vijijini. Barabara ambazo zinahitaji mwendo mrefu na zenye Kashi Kashi nyingi kufikika.

Magari ya umeme yatakayotumika Tanzania. Ni Yale ambayo Betri yake, inauwezo wa kukabiliana na mazingira yetu. Kama kutumika kutembea umbali wa maili nyingi bila kuisha Chaji.

Uwezo wa Betri zenye Nguvu ambazo zitakabiliana na matumizi ya Mtumiaji. kulingana na Uwezo wa Gari Katika mabadiliko ya Hali na Mfumo. Mfano wakati wa joto awashe kiyoyozi, au wakati wa baridi aweke joto. Au asikilize Muziki kwenye Gari yake bila kupata takishishi yoyote. Uwezo wa Betri uwe Ni Imara, Bora, Ufanisi na rahisi kuchaji.

04. Mafundi Magari wa Umeme.

Mafundi Magari wa Umeme, Hii Ni Rasimali, itakayokuwa inaishi siku Hadi siku. Kupitia Taasisi za ufundi na ujuzi tuliozazo Tanzania. tutajenga kiwanda Cha wataalamu na Mafundi wajuzi wa magari ya umeme. Kiwanda hiki msingi wake. Ni kuunda mfumo wa umeme, kwenye magari yaliyopo nchi bila kuingiza magari mapya kutoka nje yanayotumia Nishati Hiyo.

Magari yote yaliyokuwa yanatumia mfumo wa Nishati ya Mafuta zamani. Yataundwa Katika mfumo wa umeme, ili yaweze kutumia mfumo mpya wa kuchaji. kupitia Rasimali hii ya ujuzi, tutaokoa Gharama ya kuagiza Magari mapya. Magari yatakayotumia Nishati ya Umeme ni yaleyale ya mwanzo.

05. Gharama Nafuu

Msingi wa Maendeleo Ni unafuu wa Gharama, Katika uzalishaji wa Bidhaa. Uanzishwaji wa magari ya umeme yatakayotumika, Tanzania. utasaidia Gharama za bidhaa mbalimbali kuwa Nafuu Na thamani ya Pesa kuwa Juu.

•>Changamoto za Magari ya Umeme.
Teknolojia hii ya Magari ya Umeme inachangamoto ya Mtaji Duni, wa Uanzishwaji wake. Lakini Ni Nzuri, Rahisi na Bora. Katika uendeshwaji wake hapa, Tanzania.

✓Nini Kifanyike Hapa, Tanzania:
Ufunguo wa Mafanikio Ni kuanza Mapema kabla ya Muda. Wadau wa Maendeleo Kupitia Taasisi za Fedha, Wizara Husika, Taasisi za mafunzo ya elimu na ufundi. Kama Veta, NIT. Wawekeze Katika Ubunifu na Teknolojia itakayosaidia kutatua matatizo na Changamoto Katika sekta ya Usafirishaji Tanzania. Kuwepo na Uboreshwaji wa Taaluma na Mafunzo yanayotolewa kuendana na wakati. Wa namna Dunia inavyokwenda kupitia:-

01. Ubunifu.
Tafiti mbalimbali za Maendeleo zizalishe matokeo chanya Katika kubuni njia ya kutatua matatizo ya watanzania na Ulimwengu. Msingi wa ubunifu Ni udadisi wa mambo, Pia Ni Uchunguzi. Lakini Sambamba na Uchunguzi Ni utatuzi wa Changamoto. Utatuzi huu. Ni msingi wa kukua kimaendeleo na Kiuchumi Kama vile Mabara ya Ulaya, Asia na Marekani.

02. Teknolojia.
Teknolojia Ni Ulimwengu, Ulimwengu Ni watu na vitu. ili Ulimwengu uwepo unahitaji kukuwa. Kama Watu, wanavyokuwa na kuongezeka Kila kukicha. matumizi haya ya Teknolojia yanakuwa kulingana na Ongezeko la Watu, Ulimwenguni. kwahiyo, Tusisubiri. Ni kuanza Sasa. Maana Tukisubiri Tukija kuanza Tutakuta Ulimwengu umekwisha kukua na kutuacha nyuma. Hapo ndio tutazidi kuwa wa Mwisho.

03 Ujuzi
Kama ilivyo kwa Taifa Kama China Na Marekani walivyowekeza zaidi kwa raia wao. kupata ujuzi na maarifa mbalimbali Katika shughuli za Maendeleo ya Taifa. Na Tanzania ifanye ivyo kwa raia wake. Elimu iwe Ni ujuzi sio vyeti.


---Mwisho__---
 
Upvote 1
Back
Top Bottom