Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Magari ya kisasa yana dhana ya Kizimba/Ngome: ikimaanisha sehemu ya abiria imetengenezwa kwa chuma chenye nguvu zaidi kuliko magari ya zamani, hivyo basi hadi huduma za dharura zinahitaji mafunzo maalum na zana za kukata kwenye ngome ya gari la kisasa ili kuwafikia abiria katika ajali.
Na licha ya hayo, watengenezaji wa magari bado wanahitaji kufanya sehemu zingine za ngome kuwa dhaifu kidogo ili zana ziweze kuzikata.
Hapa kwa mfano kuna bodi ya Volvo V60:
Sehemu/Biti zote za njano, machungwa na nyekundu ni ngumu na haziwezi kuharibika kirahisi na hivyo kuwalinda abiria ndani ya gari, na zina nguvu zaidi kuliko chuma katika magari ya zamani.
Biti za manjano ni dhaifu vya kutosha kwa huduma za dharura kuweza kukata, lakini bado ni ngumu na zina nguvu zaidi kuliko chuma katika magari ya zamani. Ngome hii inatakiwa kustahimili uharibifu ili kuwalinda abiria dhidi ya ajali zinazoingia pindi gari linapogongwa au bodi ya gari kubanwa.
Kila kitu kingine kimetengenezwa kwa chuma laini, aluminiamu na vifaa vingine ili kuharibika na hivyo kunyonya nishati ya athari (absorb energy of an impact), au kupitisha hiyo nishati kuzunguka ngome badala ya ndani ya ngome na hivyo basi kuwalinda abiria (deflect the energy to go around the cage rather than inside the cage and thus the passengers). Na imejengwa kwa makusudi kwa kutumia nyenzo dhaifu kuliko gari za zamani.
Kwa hiyo tofauti kuu ni ya kifalsafa: magari ya zamani yalitengenezwa ili kuhimili athari kwa kutumia vyuma vigumu zaidi vya wakati huo, wakati magari ya kisasa yametengenezwa ili kudhibiti nishati ya athari (impact) kwa kutumia mchanganyiko wa vifaa dhaifu na vigumu (old cars were built to withstand impact using the strongest material of the time, while modern cars are built to manage the energy of the impact by using a combination of weak and strong materials).
Tofauti hii ya falsafa ya utengenezaji magari inaonekana wazi katika majaribio halisi ya ajali:
Chevrolet ya zamani ya 1959 imetengenezwa kwa chuma chenye nguvu zaidi wakati huo, na bado imevunjikavunjika ikiwa ni pamoja na cabin ya abiria. Pia kumbuka kuwa paneli nzima ya dashibodi, safu ya usukani na injini imesukumwa kwenye viti vya mbele, pia vipande vya kioo vilivyovunjika kutoka dirisha la mbele vimeruka kupitia chumba cha abiria. Na hilo ndilo linaloifanya kutokuwa salama - vipande vya gari huishia ndani ya abiria.
Kwa upande wa Chevrolet ya kisasa ya 2009 imemenyuka tofauti kabisa: ngome haina uharibifu kabisa. Injini imeelekezwa tena chini ya ngome, na safu ya usukani imeporomoka. Hata kama nishati ya athari inaweza kulemaza ngome kwa kiasi fulani ikigongwa moja kwa moja, haigongwi moja kwa moja kwa sababu sehemu zilizokunjamana hunyonya na kuelekeza nishati kutoka kwa ngome.
Na hii ni mbali na mifuko ya hewa (air bags) na vifaa vingine vya usalama ndani ya gari.