KERO Magari yanayobeba taka eneo la Tegeta-kwa Ndevu yanaleta kero ya foleni, wahusika wameshindwa kuliona hilo?

KERO Magari yanayobeba taka eneo la Tegeta-kwa Ndevu yanaleta kero ya foleni, wahusika wameshindwa kuliona hilo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Kuna maeneo katika Jiji la Dar es Salaam unakutana na foleni lakini ukifuatilia kwa umakini kuna wakati unagundua kuna uzembe wa uwajibikaji na kukosekana kwa ubunifu kwa baadhi ya watendaji waliopewa dhamana.

Eneo ambalo hasa limenifanya kuchukua uamuzi wa kuandika, ni pale eneo la Tegeta-kwa Ndevu kuna muda kunakuwepo foleni ya mara kwa mara, baada ya kufuatilia foleni nimegundua inachangiwa na magari ya uchafu ambayo ufika maeneo hayo kubeba uchafu ambao unarundikwa kando ya barabara.

Screenshot 2024-10-11 133858.png

Screenshot 2024-10-11 133917.png

Kibaya zaidi shughuli hizo wahusika wanazifanya wakati ambao barabara zipo bize watu wakiwa wanaenda kazini au wakati mwingine wakiwa wanatoka kwenye majukumu ya hapa na pale.

Kuna wakati najiuliza kwanini, wahusika ambao ni mamlaka zinazosimamia usafi zitafute eneo rafiki na rasmi kwa ajili ya magari ya taka kupaki kupakia uchafu, kuliko utaratibu wa taka kurundikwa kando ya barabara jambo ambalo linaleta foleni kutokana na magari kusimama barabarani muda mrefu.

Basi kama utaratibu huo umewashinda kwanini wasifanye shughuli hizo wakati wa usiku ambapo njia hiyo inakuwa haipo bize sana, wakabeba taka hizo kwenye maeneo hayo sambamba na mengine yenye kero ya aina hiyo.

Wahusika kubariki shughuli hizo kuendelea kwenye barabara hiyo ya kimkakati (Bagamoyo Road) haswa wakati wa asubuhi na jioni ni kukosa uwajibikaji stahiki.

Screenshot 2024-10-11 134114.png

Screenshot 2024-10-11 134102.png

Pia soma ~ Eneo la Tegeta - Kwa ndevu uchafu unarundikwa eneo la barabara kama dampo, wasimamizi wako wapi?
 
Poleni sana na hapo ujenzi wa mwendokasi haujaanza hapo ,ukianza nadhani itakuwa balaa itabidi mpitie njia ya chini Ununio-Bahari Beach-Mtongani -kwa Mwannyange/Juliana-Kwa Kusaga /Kwa Zena.
 
Back
Top Bottom