Wakuu habarini
Kwanza niwape pole na Majukumu,
Naomba kujua kwa wataalamu wa Magari kuhusu Aina za Magari toka kampuni tofauti na toyota ambazo zipo miaka mingi mfano Volkswagen, Honda, Nissan, Mazda, Ford, Benz, Suzuki nk. Je magari yao ni mabovu, hayaaminiki au hayana spea hapa Tanzania?
Kwanini Toyota pamoja na kuwa gari zao ni za gereji kila siku kwa sababu ya spare parts feki bado zinauza kwa soko la Tanzania.
Je ni kwanini kampuni nyingine hazifurukuti au n mtazamo wa Watanzania tu?
Naomba nipatiwe ufafanuzi.
Kuna sababu nyingi. Kwanza, ni rahisi saana kununua magari ya Asia, hasa Japan kwa sababu yanatengenezwa kwa wingi saana huko, na sheria lazo hasa za bima zinawabana wale wenye magari mazee. Hivyo wanalazimika kuyauza kwa bei ya chini kiasi kwamba watu wengi wa Afrika wanaweza kuyanunua.
Pili, gari za Japan kama Toyota ni ngumu saana, tofauti na unavyofikiria. Gari nyingi unazoziona Tanzania leo zilishasitishwa uzalishaji wake karibu miaka 10 na zaidi. Mfano, Altezza model ya mwisho ilizalishwa mwaka 2005, more than 10 years ago, ila zinaweza kuvumilia kutumika kwenye hali ngumu, na spare parts fake.
Gari za Ulaya ni ngumu pia, hasa gari za Ujerumani mf BMW, Mercedes na Audi na VW. Ni kati ya gari zinazotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu. Tatizo lake ni kwamba ziko very
sophisticated (za kisasa zaidi) siku nyingi ukilinganisha na gari tulizozoea, sasa kwa maisha ya mafundi wa kubahatisha na spare parts fake inakua vigumu saana kuzitumia kwa mazingira yetu. Ndio maana unaona watu wanaziogopa.
Vile vile spare parts zinaonekana ni ghalama kidogo sababu wazalishaji wa spare fake ni wanabanwa saana kuziingiza Ulaya na Marekani ambako gari za Ulaya zinatumika zaidi, so mwisho wa siku soko la bidhaa zao linakua dogo kulinganisha na magari ya Japan.
So, hitimisho langu ni kwamba,
most Toyotas and other Japanese cars ni very reliable, and less complex to maintain kwenye mazingira magumu kama Africa. European cars are very well made, quite a number of them sio very reliable hasa kwa mazingira magumu kama Afrika, maana gari hizo zina mifumo complex ambayo inabidi ilindwe na kutunzwa vyema.