Ab-Titchaz
JF-Expert Member
- Jan 30, 2008
- 14,630
- 4,253
Magavana wa CORD kuzuru Amerika kukutana na wawekezaji
Imepakiwa - Wednesday, July 17 2013 at 08:03
Kwa Mukhtasari:
Magavana wa muungano wa CORD wanatarajiwa kuzuru Amerika na Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi huu kukutana na wawekezaji.
MAGAVANA wa muungano wa Cord wanatarajiwa kuzuru Amerika na Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi huu kukutana na wawekezaji watarajiwa.
Duru kutoka kwa muungano huo zimedokeza kuwa magavana wa muungano huo wamegawanywa kwa makundi matatu ambayo yatafanya ziara za siku mbili kukutana na Wakenya wanaoishi nje katika harakati za kuchochea maendeleo katika kaunti zao.
Kundi la kwanza litaelekea Texas ilhali la pili litaenda Philadelphia na la mwisho Johannesburg, Afrika Kusini ambapo watafanya mikutano na majadiliano na wawekezaji.
Imeripotiwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa Cord Raila Odinga ndiye aliyeomba na kupata nafasi ya magavana hao kukutana na wawekezaji.
Gavana wa Siaya Cornel Rasanga ambaye ni miongoni ya wale watakaoenda Texas, alithibitisha kwamba watasafiri Amerika na kwamba kundi lake litakuwa na magavana 12.
"Ni kweli tutasafiri Texas na lengo letu kuu ni kukutana na wawekezaji na kuwavutia kwa kaunti zetu," alisema Bw Rasanga katika mahojiano ya simu.
Duru za karibu na mipango hiyo zilifichua kuwa magavana hao watajifadhili wenyewe katika ziara hizo.
Mikutano
"Ziara hiyo ni za kutafuta watu ambao wanaweza kuwekeza kwa lengo la kuwavutia kutumia nafasi kadha ambazo zinapatikana katika kaunti tofauti," duru hiyo iliongeza.
Hatua hii imejiri mwezi moja baada ya magavana kutoka Rift Valley ambao ni wa chama cha United Republican Party (URP) kurejea nchini kutoka kwa ziara ya juma moja Amerika ambapo walihudhuria mikutano kadha na wawekezaji watarajiwa.
Gavana wa Bomet Isaac Ruto aliongoza ujumbe ambao ulijumuisha gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago Cleaophas Lagat wa Nandi na naibu gavana wa Elgeyo-Marakwet Gabriel Lagat.
Magavana wa CORD kuzuru Amerika kukutana na wawekezaji - HABARI ZA SIASA - swahilihub.com