Magavana wamtaka Rais Kenyatta kutangaza Saratani kuwa janga la kitaifa

Magavana wamtaka Rais Kenyatta kutangaza Saratani kuwa janga la kitaifa

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Magavana nchini Kenya wamemtaka Rais Kenyatta autangaze ugonjwa wa Kansa kuwa janga la kitaifa.

Taarifa iliyotolewa kupitia Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Wycliffe Oparanya siku ya Jumamosi inaeleza kuwa wakati Wakenya wakiendelea kuomboleza vifo vya Gavana wa Bomet, Dkt. Joyce Laboso, Mbunge wa Kibra, Ken Okoth na aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Safarivom, Bob Collymore, uhatari wa ugonjwa huo umekuwa dhahiri zaidi.

Kulingana na ripoti ya Taasisi ya Taifa ya Kansa, ugonjwa huo umeenea zaidi Kisumu, Kakamega, Nyeri, Nakuru, Bomet na Uasin-Gishu.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa changamoto kuu ni gharama ya matibabu kwa wagonjwa ambapo mionzi hugharimu Ksh. 500 hadi 1,000 na dawa hugharimu Ksh. 6,000 hadi 600,000 katika hospitali za Serikali.

Wameitaka Serikali kuangalia upya suala hili kwa sababu gharama hizi ni kubwa kwa Mkenya mwenye kipato cha wastani

========

Governors have called on President Uhuru Kenyatta to declare cancer a national disaster.

Council of Governors Chairman Wycliffe Oparanya on Saturday said that as Kenyans come to terms with the death Bomet Governor Dr Joyce Laboso, Kibra MP Ken Okoth and Safaricom former CEO Bob Collymore, a chilling realisation was sweeping the country about their vulnerability to the disease.

"According to the latest report by the National Cancer Institute of Kenya, cancer is most prevalent in Kisumu, Kakamega, Nyeri, Nakuru, Bomet and Uasin-Gishu counties, " Mr Oparanya said in a statement.

The key challenge being the cost implication it has on the victims, Mr Oparanya said.

"Patients pay between Sh500 to Sh1, 000 per session for radiotherapy in state-run hospitals while chemotherapy costs Sh6, 000 to Sh600, 000, depending on the drug used. This is not achievable for the average Kenyan and we need to rethink these costs," the Kakamega governor said.

Source: Nation.co.ke
 
Pole yao kwa kweli.

Huku Tanzania mtetezi wa wanyonge JPM kafanya kuwa BURE na matibabu yake ni viwango vya kimataifa

Ni nyumbu tu wanamsema JPM vibaya ila ukiona habari kama hizi toka kwengine ndio unaona umuhimu wa ulichonacho

Dah utayasikia yakiropoka mambo ya kipumbavu eti uhuru wa kujieleza, wakati huo huko tweeter wakimporomoshea matusi ya kila aina na bado wapo safe ila habari kama hizi wanazipa kisogo.

Watanzania wanyonge wanaopata matibabu ya saratani pale ocean Road na Bugando ukiwaeleza huo upumbavu kuhusu magufuli wanaweza kukumeza
 
Uzuri ni wachache sana, majority ya Watanzania wanamuelewa vizuri na kulijua hilo utaona 2020

Au kama una muda tembelea youtube zile sauti zilizoliki za wale wazee matapeli kisha soma comments Watanzania walivyochafukwa ndio utajua huyu jamaa anakubalika

Nimeona nisikuambia uangalie maelfu ya watu wanaojitokeza kwenye misafara yake na mikutano sababu wanasema kwamba wanasombwa pahala.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Wanasiasa bwana!! Yaani ugonjwa baada ya kuanza kuwaua na wao ndyo wanastuka kuwa utangazwe janga la taifa.....ulipokuwa unawaua wananchi wa kawaida waliona sio tatizo!
 
Waanze kampeni ya mfumo wa maisha hasa ulaji ndo unachangia sana kuongezeka kwa kansa
 
Inaonesha wala samaki kwa sehemu kubwa niwaathirika
 
Dah utayasikia yakiropoka mambo ya kipumbavu eti uhuru wa kujieleza, wakati huo huko tweeter wakimporomoshea matusi ya kila aina na bado wapo safe ila habari kama hizi wanazipa kisogo.

Watanzania wanyonge wanaopata matibabu ya saratani pale ocean Road na Bugando ukiwaeleza huo upumbavu kuhusu magufuli wanaweza kukumeza
Matibabu yanayotolewa ni duni na wagonjwa wengi hufariki! Wengi hukaa foleni ndefu ya kupata hiyo mionzi! Tembelea Oshen Rodi ushuhudie mwenyewe! Acheni siasa!
 
Uzuri ni wachache sana, majority ya Watanzania wanamuelewa vizuri na kulijua hilo utaona 2020

Au kama una muda tembelea youtube zile sauti zilizoliki za wale wazee matapeli kisha soma comments Watanzania walivyochafukwa ndio utajua huyu jamaa anakubalika

Nimeona nisikuambia uangalie maelfu ya watu wanaojitokeza kwenye misafara yake na mikutano sababu wanasema kwamba wanasombwa pahala.
Wadanganyeni wasiojua! Kama umewahi kufika oshen rodi na kushuhudia, huwezi pongeza ujinga! Kama huna pesa ya kulipia pale, wewe ni marehemu mtarajiwa! Msidanganye!
 
Wadanganyeni wasiojua! Kama umewahi kufika oshen rodi na kushuhudia, huwezi pongeza ujinga! Kama huna pesa ya kulipia pale, wewe ni marehemu mtarajiwa! Msidanganye!
Vipimo vyote na tiba ni bure acha upotoshaji, hata elimu ni bure lakini sio kama serikali itamgharamia mwanao mpaka chakula kuna wigo hiyo bure haifiki.
 
Vipimo vyote na tiba ni bure acha upotoshaji, hata elimu ni bure lakini sio kama serikali itamgharamia mwanao mpaka chakula kuna wigo hiyo bure haifiki.
Amekuelewa ana taka kutanua mapafu kwa porojo ambazo hazijui
 
Back
Top Bottom