Magereza Kiteto yachapwa 1-0 na Polisi

Magereza Kiteto yachapwa 1-0 na Polisi

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Ile mechi ya kirafiki kati ya Jeshi la Polisi Kiteto na Magereza, mshindi kuibuka na mbuzi Mnyama, timu ya Polisi imeibuka kidedea.

Mpira ulikuwa patashika nguo kuchanika, baada ya mbuzi huyo kuonekana kiwanjani akirandaranda kula nyasi akisubiria mshindi Wa kimnyakua.

Katika dk 37 vijana Wa Polisi Kiteto waliwanyanyua washabiki wao kwa kupachika mpira katika nyavu za timu ya Magereza

Hadi kipindi cha pili kinamalizika pamoja na kurupushani za hapa na pale timu ya Magereza ilishindwa kurejesha bao hilo

Akikabidhi zawadi hizo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Walaya ya Kiteto Tamimu Kambona, alipongea muandaaji wa mchezo huo ambaye alikuwa Jeshi la Polisi Kiteto chini ya OCD Luoga

Alisema utaratimu huu ni mwema wakuigwa kwani michezo ni udugu na unajenga urafiki sambamba na kuibua vipaji.

Kwa upande wa Mkuu wa Polisi Kiteto SP Luoga alisema nia ya Jeshi la Polisi ni kujenga mahusiano mema na majeshi mengine pamoja na RAIA.

Huku Patrick Kimaro (Sabasita) akisema michezo hiyo itaendelea huku akitaka pia wakulima na wafugaji nao wawe na timu za mpira kujenga mahusiano mema.

Mwisho.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom