esterphilipi
Member
- Aug 13, 2022
- 5
- 4
Kumekuwepo na changamoto ya wahalifu wengi (japo sio wote) kuongeza matukio ya kihalifu na tabia zisizo za kimaadili pindi wanapotoka magerezani baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao. Ambaye alikua havuti sigara anatoka anavuta sigara, aliyekua hanywi pombe anatoka anakunywa pombe, aliyekua mwizi wa kuku anatoka jambazi wa kuvunja maduka ya watu. Kwa ufupi ni kwamba ni kama wanapanda viwango vya uhalifu.
Swali la kujiuliza ni je, magereza nchini yamekua vyuo vya kuzalisha wahalifu? Tunatambua kwamba magereza ni sehemu ya kumtenga muhalifu na jamii yake hivyo kumfanya kujutia makosa yake na kujirekebisha au kuacha uhalifu. Lakini ni kwanini baadhi ya wafungwa kuongeza matukio ya kihalifu pindi watokapo gerezani? Ni vizuri kutafutia jibu hili na kuweka mikakati mizuri katika kutatua changamoto hii.
Ni kwanini magereza yasifanywe kama sehemu ya kufufua ndoto za wahalifu, huenda pia ikawa kama njia ya utatuzi wa jambo hili. Hakuna asiye na ndoto, pia hakuna mwenye ndoto ya kufanya uhalifu lakini inapotokea changamoto katika kutimiza ndoto zake mtu hujikuta kujiingiza kwenye matukio ya kihalifu na tabia zisizo na maadili hali inayopelekea kuishia gerezani. Huko nako hujikuta akijifunza/kufundishwa mambo mengi zaidi yasiyo ya kimaadili.
Kinachofanya mtu kuongeza uhalifu na tabia zisizo na maadili pindi anapotoka gerezani ni kutokana na gereza kuzidi kudidimiza ndoto zake na hivyo kupelekea kujifunza kutoka kwa wahalifu wakubwa zaidi anaokutana nao gerezani. Jibu rahisi ni kua wengine hupata โconnectionโ za uhalifu zaidi pindi wawapo gerezani. Itakua jambo jema kama itawekwa mikakati ya kupambana na hili kwa kuwakumbushia ndoto zao na kuwasaidia njia zitakazofufua ndoto hizo
Yafanyike yafuatayo ili kufufua ndoto za wahalifu magerezani,

1. Magereza yatambue pia wahalifu wana vipaji vyao,
Hivyo basi, mazingira ya magereza yatengenezwe kuwawezesha wafungwa kupata muda walau mara mojamoja waweze kushiriki kwenye michezo mbalimbali kama, mpira wa miguu, kikapu, netiboli, riadha, muziki, nakadhalika. Hii itasaidia kuendeleza na kufufua vipaji vya baadhi ya wafungwa na kuwafanya kuweza kuvitumia pindi watakapomaliza vifungo vyao.
2. Mafunzo ya fani mbalimbali yafundishwe gerezani,
Hasahasa mafunzo ya ufundi kama uashi, useremala, ususi, ushonaji wa nguo, pia ufundi wa magari, umeme, bomba nakadhalika. Itawasaidia kupata ujuzi ambao utawafanya waweze hata kupata ajira pindi wanapomaliza vifungo vyao.
3. Kuweka wanasaikolojia kwenye magereza,
Wafungwa wengi wanahitaji ushauri nasaha ili kuwapa tumaini la maisha kitu kitakachowasaidia kutokutenda uhalifu na pia kubadili mitazamo yao pindi wanapotoka gerezani. Wapo wenye mipango ya kulipiza kisasi watakapotoka gerezani ila watakapopatiwa ushauri nasaha itawasaidia kubadili mawazo yao. Hivyo inabidi walau kabla mfungwa hajamaliza kifungo chake awe ameonana na mwanasaikolojia kwa zaidi ya mara moja.
4. Kuendesha semina mbalimbali kwa wafungwa,
Iwekwe ratiba ya kutoa semina kwa wafungwa, semina zitakazowafungua akili na kuwawezesha kuweza kupambana na maisha bila kuvunja sheria za nchi. Pia semina zitakazowasaidia kuwapa ujasiri wa kujiunga na kushirikiana tena na wanajamii pindi watakaporudi uraiani.
5. Kuwawezesha kupata huduma za kiroho,
Uwekwe utaratibu wa kuwaruhusu watumishi wa kidini kwa ratiba maalumu kuweza kuingia magerezani na kushiriki na wafungwa katika huduma za kidini. Itawapa hofu ya Mungu wasio na hofu, itawasaidi wenye kuhitaji kutubu kuweza kutubu. Itasaidia pia kuondoa roho chafu za uhalifu rohoni mwao na kuwawezesha kuacha uhalifu
Faida zitakazotokana na jambo hili,
Licha ya mambo haya kusaidia katika kupunguza uhalifu pindi wafungwa watakapomaliza mafunzo yao ila pia itasaidia katika mambo mbalimbali kama;
Faida zitakazotokana na jambo hili,
Licha ya mambo haya kusaidia katika kupunguza uhalifu pindi wafungwa watakapomaliza mafunzo yao ila pia itasaidia katika mambo mbalimbali kama;
1. Magereza kujiingizia vipato zaidi,
Kutokana na kutengeneza wafungwa wengi wenye fani mbalimbali, wataweza kufungua shughuli za kuwaingizia kipato. Shughuli kama ushonaji wa nguo, ufundi wa magari nakadhalika utawawezesha kutoa huduma hata kwa wanajamii wanaohitaji huduma hizo jambo litakasaidia magereza kujiingizia kipato.
2. Kupunguza uhalifu mitaani,
Wafungwa watakapopatiwa semina pamoja na ushauri basi hata uwezekano wao wa kutenda uhalifu utapungua kwa kiasi kikubwa,. Hii itasaidia kupunguza matukio ya kihalifu mtaani. Pia wapo watakaotoka na fani zitakazowasaidia kujiingizia kipato na kuacha kutumia njia haramu kujiingizia kipato.
3. Kutengeneza kizazi kinachojali utu,
Kutokana na kupatiwa huduma za kiroho, semina na pia ushauri nasaha, kitu ambacho hata mtaani ni ngumu kupatiwa. Itawasaidia kutambua na kujali utu wa wengine. Watatambua thamani yao kwenye jamii, jambo litakalowafanya kutambua pia thamani ya watu wengine. Hii itawafanya wale waliokua wakifanya matukio yanayowaumiza wengine kuingiwa na roho ya huruma na kuachana na vitendo hivyo.
Hivyo basi, magereza yasitumike tu kama sehemu ya kuwaadhibu wafungwa, wanapoadhibiwa basi wawezeshwe kutambua waliyoyatenda sio sawa. Wakitambua sio sawa wapewe elimu ya kuepuka kuyatenda tena yale waliyotenda mwanzo. Wafungwa nao ni binadamu, hakuna binadamu anayezaliwa akiwa mhalifu, uhalifu unapatikana kutokana na mambo mtu anayokumbana nayo kwenye mazingira wakati wa ukuaji wake. Jambo la muhimu ni kumsaidia aweze kuachana na uhalifu na atambue aliyoyafanya hayafai kwenye jamii.

Upvote
8