Magereza yote kuwekwa vifaa vya upekuzi, CCTV

Magereza yote kuwekwa vifaa vya upekuzi, CCTV

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
JESHI la Magereza linakusudia kuongeza vifaa vya upekuzi magerezani na kufunga kamera za usalama za CCTV, ili kubaini vitendo viovu vinavyofanyika ndani ya magereza hayo.

Hayo yalisemwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati ikijibu swali la Mbunge Viti Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF), aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuzuia vitendo viovu magerezani.

Wizara hiyo ilisema pamoja na kufunga vifaa hivyo, pia itaendelea kufuata sheria na kanuni ambazo zilipitishwa na Bunge na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaohusika kufanya vitendo viovu magerezani.

“Ni ukweli kwamba, nyakati kadhaa kumekuwapo na vitendo viovu magerezani, mathalani askari kuwa na mahusiano mabaya na mfungwa, uingizaji wa vitu visivyoruhusiwa magerezani, matumizi mabaya ya nguvu dhidi ya wafungwa na vitendo hivyo vimekuwa vikidhibitiwa.”

“Vitendo vingine ambavyo vimekuwa vikidhibitiwa ni wafungwa kujaribu kutoroka, kupigana, kutoeleana lugha za matusi na kuharibu mali ya gereza,” ilisema.

Wizara hiyo ilisema sheria na kanuni zimeainisha aina ya makosa, hatua na adhabu zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya ofisa/askari wa Magereza, mfungwa/ mahabusu, pale inapothibitika amefanya vitendo hivyo gerezani.


Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom