James Godfrey
Member
- Aug 27, 2022
- 19
- 12
Inatisha na kusikitisha jinsi changamoto za sekta ya afya zinavyoathiri watu kote ulimwenguni, Tanzania nchi yangu nayo haijaachwa nyuma na janga hili linalokua kila uchwao, linaloteka vichwa vya habari duniani kote, umekua kama wimbo unaojirudia masikioni mwetu kila siku, bila ubishi wengi wetu ni wahanga kwa namna moja au nyingine wa janga hili linaloikumba sekta hii nyeti kabisa, ambayo kila mtanzania anatamani kuona ikiboreshwa, maana linapokuja swala la afya hapa unagusa uhai wa mtu, kitu ambacho binadamu yeyote yupo tayari kukilinda kwa gharama yoyote ile, ndipo ninapomuelewa yule muhenga aliyesema "afya bora ni mali kuliko dhahabu".
Matatizo yanayoikumba sekta ya afya ni mengi sana natamani hata niandike waraka mrefu sana lakini nimepewa ukurasa mmoja tu hivyo sina budi kuutumia vizuri, napenda kuutumia ukurasa huu kuandika juu ya changamoto moja kati ya nyingi zinazoikumba sekta ya afya, changamoto ya usahihi wa vipimo vya mahabara katika hospitali nchini, makosa katika vipimo yanaweza kuwa na matokeo mabaya, ikiwa ni pamoja na uchunguzi usio sahihi, matibabu yasiyofaa, hata kifo kwa mgojwa.Kwa maono yangu Tanzania tumeachwa nyuma kwa kiasi fulani na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika vipimo vipya vya ulimwengu wa kileo. Maendeleo katika ulimwengu wa teknolojia ya upimaji na vipimo vya mahabara yanatupa tumaini jipya na endelevu la kupunguza hatari zinazohusiana na vipimo visivyo sahihi hivyo kuhakikisha usalama na afya ya mgonjwa.
Picha ikionyesha changamoto katika upimaji chanzo Google photos
Kabla sijaanza kuelezea vipimo hivi vya ulimwengu wa kileo vinavyotumia sayansi ya "molecular biology na biotechnology" hebu sikia hadithi hii fupi, "alikuepo mama mwenye watoto wawili wadogo aliyekua akiugua ugonjwa asioufahamu , akaenda kituo cha afya akapima, baadae kidogo akaambiwa "mama hatuoni kama una ugonjwa itakua ni mchafuko tu wa damu" hayo ni maneno ya daktari baada yakupata majibu ya vipimo vya mahabara, mama huyo akarudi nyumbani huku akiwa mwenye furaha kwamba yeye si mgonjwa, baada ya mwaka kupita hali ya mama yule ikazidi kuwa mbaya, afya yake ikazidi kuzorota ikabidi apelekwe hospitali ya wilaya alipofika huko akafanyiwa tena vipimo, majibu yakaonyesha mama yule haumwi, Lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya ilibidi apewe uhamisho(transfer) kwenda hospitali ya Rufaa ya Kanda yake, alipofika akagundulika mama yule anaumwa saratani ya mapafu tena ipo katika hatua za mwisho kabisa, hivyo daktari akashauri ahamishiwe hospitali ya ocean road jijini dar es salaam, hospitali iliyotengwa kwajili ya wagonjwa wa Saratani nchini, baada ya kufika hospitali hali yake ikazidi kuwa mbaya zaidi, siku nne baadae mama yule akapoteza maisha, ilikuwa ni simanzi kubwa kwa familia ya mama yule.
Hii inaweza kuwa hadithi kama nilivyotangulia kusema hapo juu lakini kiuhalisia hii sio hadithi wala stori ya kufikirika hii ni hali inayowakumba wagonjwa wengi hapa nchini, wengine wanapoteza maisha ili hali kulikua na uwezo wa kuyanusuru.
Kupitia hadithi hiyo hapo juu hapa tunaweza kuona baadhi ya changamoto katika hospitali zetu pale linapokuja swala la upatikanaji wa vipimo, ufanisi wa vipimo hivyo na ubora wa majibu ya vipimo hivyo, kama kalamu yangu inavyofafanua hapo chini
1.UHABA WA VIPIMO KATIKA HOSPITALI ZA NGAZI ZA CHINI
Ndio maana mama yule hakuonekana akiumwa alipofika hospitali ya kijijini kwake hata ya wilayani kwake kutokana na kukosekana kwa vifaa vyenye uwezo wakugundua viashiria vya ugonjwa hata katika hatua za mwanzoni kabsa.
2.VIPIMO KUTOA MAJIBU YASIYO SAHIHI(UFANISI WA VIPIMO)
Mama yule alipimwa kweli Lakini vipimo bado havikuweza kutambua viashiria vya ugonjwa wa saratani, hii inaweza kutokana na vipimo hivyo kutumia teknolojia ya zamani ambayo kwa kiasi fulani inapata tabu katika utambuzi wa baadhi ya magonjwa haswa katika hatua za awali
3.UHABA WA HOSPITALI ZENYE VIPIMO VYA KIBINGWA
Sababu ya mama yule kusafirishwa kilometa nyingi kutoka kijijini kwake hadi Dar es salaam ni sababu ya uhaba wa hospitali za aina ya ocean road hapa Tanzania, mimi siamini kama ni kweli hospitali hii moja inaweza kukidhi mahitaji ya watu Zaid ya milioni 60 kutoka pande zote za Tanzania, maana sisi wote ni wagonjwa watarajiwa.
Kutokana na changamoto kama hizi ndipo nilipoona Kuna haja ya wizara ya afya kukubali na kuanzisha matumizi ya vipimo vinavyotumia teknolojia hii mpya katika hospitali zetu, hata zile za ngazi za chini, maana naona inaweza kutatua changoto zote hapo juu.
Je Vipimo vinavyotumia teknolojia ya molecular biology ni vipi na vinafanyaje kazi? Nazani bado mwandishi sijalijibu swali hili.
Inaweza kuonekana kama ni vifaa vya ajabu lakini amini usiamini vifaa hivi vipo nchini, lakini matumizi yake ni makubwa katika taasisi zinazojihusisha na maswala ya utafiti, kama vile National Institute of medical research(NIMR), Ifakara Health Institute(IHI), Kilimanjaro clinical research institute(KCRI) nakadhalika pia katika hospitali chache hapa nchini.
Naweza kuelezea sayansi inayotumika katika vifaa hivi kama ifwatavyo,
Kwa lugha rahisi kabisa, kama vile ambavyo ukinunua bidhaa dukani unakuta kuna lebo imebandikwa ambapo ukifanikiwa kuiisoma utafahamu taarifa zote za bidhaa hiyo kuanzia tarehe iliyotengenezwa, tarehe ya mwisho wa matumizi, vilivyotumika kuitengenezea hata faida za bidhaa hiyo, vivyo hivyo mwili wa binadamu una chembe chembe ndogo sana kama vile DNA, RNA, proteins n.k ambapo chembe hizi ndogo zimebeba taarifa zote zilizopo kwenye mwili wa binadamu(Hata taarifa zote za kiafya) hivyo tukipata njia ya kuweza kusoma chembe hizo tunaweza kujua taarifa zote za mwili wa binadamu(kujua afya ya mtu), ndipo wanasayansi wakabuni vifaa ambavyo vinaweza kusoma taarifa hizi, ndipo tukapata vifaa vinavyotumia teknolojia ya molecular biology.Hivyo vifaa hivi vinapotumiwa katika mahabara za hospitali hufanya kazi ya kuchunguza chembe hizo ndogo zilizozikusanywa kutoka katika sampuli kama vile mate, damu, kinyesi, mkojo n.k kuona kama kuna dalili au viashiria vyovyote vya ugonjwa au viashiria vya hatari yoyote ya kiafya kwa mgonjwa.
Picha ikionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumia teknolojia mpya, chanzo Google photos
FAIDA YA VIFAA HIVI KATIKA KUPIMA NA KUTOA MAJIBU SAHIHI
1. USAHIHI: Vifaa hivi vina usahihi mkubwa katika kupima sampuli za wagonjwa, vinapunguza makosa ya kibinadamu na kuongeza usalama wa mgonjwa.
2. UFANISI: Vifaa hivi vina uwezo wa kugundua ugonjwa hata katika hatua za awali, kuwezesha matibabu mapema na kupunguza vifo vinavyoepukika.
3.AJIRA: Matumizi ya vifaa hivi yataongeza fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania, kwa sababu katika vyuo vyetu hapa nchini vijana wetu wanafundishwa kuhusu teknolojia hii mpya, lakini kutokana na kwamba teknolojia hii imebakia katika taasisi za utafiti ambazo ni chache hapa nchini ukilinganisha na idadi ya vijana wanaomaliza vyuo kila mwaka hivyo vijana wengi wanabaki mtaani bila ajira, lakini teknolojia hii ikikubalika na kutumika katika hospitali za ngazi zote hapa nchini fursa za ajira kwa vijana hawa zitaongezeka hivyo kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini.

Upvote
11