Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Ewe Kivuyo mwema, nduguyo nakusalimu
Jangwani hali si njema, nawe pia u-adimu
Mpira si lelemama, ligi hii si ya chandimu
Uwapi Ewe Kivuyo Mwema?
Habari zimenifika, umejificha Nida
Ni yepi yamekufika, usifiche yako shida
Sie sukani kushika,Yanga mmejawa husda
Uwapi Ewe Kivuyo Mwema?
Kalamu naweka chini, nasubiri lako jibu
Wala usibaki mitini, haraka uje na jibu
Simba timu ya mjini, Yanga mwefikwa aibu
Uwapi Ewe Kivuyo Mwema?
maggid