Ndugu zangu,
Usiku huu nime-google jina langu ndipo nimekutana na habari hii. Ukweli imeniburudisha na kunipa elimu pia. Ama hakika, ishi ujionee na ujifunze kutoka kwa wanadamu wenzako.
Nalaumiwa kwa kuwa Mjengwablog haiku-post picha za tamasha la Anti- Virus. Na ni jana tu nimenunua kitabu cha Mr. Sugu kuhusu maisha yake- From Streets to The parliament.
Ndugu zangu,
Mie naishi na kufanya kazi Iringa. Ni mahali ambapo hata mtandao wakati mwingine ni wa shida. Na kublogu huku tunajitolea tu. Hata matangazo ya maana hatuna, Tunatumia senti za mifukoni mwetu. Na kazi ya kublogu naifanya nikiwa na wakati ziada.
Tena siku hizi nina mwanafunzi wangu aliye Dar na anayenisaidia wakati mwingine kuifanya kazi hiyo. Kuhusu picha za tamasha hilo linalosemwa nami niliziona zimetundikwa kwenye Mjengwablog.com na mwanafunzi wangu huyo.
Niwahakikishie, kuwa Mjengwablog ni blogu huru. Haijapata kununuliwa na haitakuja kununuliwa kufanya kazi za kishabiki. Na mimi kama mmiliki wa blogu ndivyo nilivyo. Sijapata kununuliwa na sitakuja kununuliwa nimfanyie mtu kazi ya kishabiki na isiyo na maslahi ya kitaifa.
Pamoja na yote hayo. Niseme tu, kwa hata mabaya yaliyoandikwa hapa juu yangu, sina kinyongo na mtu. Na nirudie, niliyosoma hapa usiku huu yameniburudisha pia. Nimebaki nikicheka mwenyewe kuona jinsi watu wanavyonifikiria, kunituhumu na kunihukumu, bila hata kunipa nafasi ya kunisikiliza.
Nawatakia usiku mwema.
Maggid,
Iringa.
.