Maghorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo

Nakubaliana nawewe, tusubiri majanga mengine yatakayokuwa yamesababishwa na UZEMBE sio janga moja

Na bado yatajengwa mengine kizembe zembe tu kwasababu hakuna mamlaka yenye nguvu ya kusimamia hili Tanzania

Nchi ya maajabu hii
 
Uzi wa 2013, miaka 11 sasa....Mola aepushe zaidi majanga, awape nafuu majeruhi, awape kauli thabit waliotangulia mbele ya haki kwa kadhia hii ...awape subra ndugu na jamaa walio patwa na changamoto
Hizo dua wala hazisaidii, huyo unaemuita Mola alishawapa watu wake akili ndio maana wakagundua kua kuna majengo yanayokaribia kuporomoka.
Sasa kama hawakuchukua hatua stahiki Mola anahusikaje hapa? kauli thabit sijui subra vyote ni nonsense!!
 
Mkuu una hangover!?
Mleta mada hakutabiri bali alileta ripoti ya ukaguzi na ripoti imeanza kutoa majibu.
 
Vibali vya ujenzi nani anatoaaaaaa,tena unakuta wameweka na vibao kabisa kua mkandarasi ameizinishwa so why now????
 
Wanachunguza baada ya Ujenzi badala ya wakati wa ujenzi...., Always Reactive and Never Pro Active..., ila na hili tutalipigia kelele litapita mpaka pale janga lingine tupige tena kelele.... ili tuajiri tena kampuni ifanye uchunguzi
 

Hii ni hatari sana, kumbe uchunguzi ulishawahi kufanywa na kasoro kuibuliwa! Naamini kama kasoro hizi zingefanyiwa kazi basi pengine haya yasingetokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…