Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CONDESTER SICHALWE AKABIDHI MAGODORO 30 (MILIONI 2.5) KWA WANAWAKE UWT WILAYA YA MOMBA
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe tarehe 26 Julai, 2023 amekutana na Wanawake wa UWT Wilaya ya Momba na kuwakabidhi Magodoro 30 yenye thamani ya Shilingi Milioni 2,505,000
Mhe.Condester Sichalwe aliambatana na Maafisa Kilimo wa Wilaya ya Momba kwaajili ya kutoa elimu kuhusu mambo yote ya Kilimo kwani wananchi wanahitaji elimu ya Kilimo ili waweze kuwa na Kilimo chenye tija
Mhe. Condester Sichalwe amewataka Viongozi hao kuwa Mabalozi wazuri kwa kuitisha mikutano ya hadhara na kuwapa taarifa mbalimbali za uzalishaji Kilimo waliyoipata na amewaomba Viongozi wa UWT kuwasiliana na Maafisa Kilimo Wilaya ya Momba kwani wapo tayari muda wowote kwenda kuwasikiliza na kuwapa Elimu ya Kilimo chenye tija.
Aidha, Mhe. Condester Sichalwe alipata chakula cha pamoja cha mchana na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Momba ambao walimshukuru sana Mbunge Condester kwa kuwapa semina ya Kilimo na kuahidi kufanyia kazi elimu waliyoipata
Mhe. Condester Sichalwe amewashukuru UWT Momba kwa ushirikiano wanaompa na kuwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuunga mkono juhudi za Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan