Magolikipa wa NBCPL wanaweza kujifunza mambo kadhaa kutoka kwa Diara. Katika mechi ya jana kati ya Yanga vs JKT kuna mipira ilipigwa kwa Diara ikaokolewa vizuri, lakini ikawa na madhara kwa golikipa wa JKT.
Baadhi ya mambo ambayo magolikipa wengine wanaweza kujifunza kutoka kwa Diara:
1. Golikipa kurudishiwa pasi na kuipiga tena kwa mguu
Hapa inabidi magolikipa wafanye mazoezi ya kuuchezea mpira kwa miguu ili iwe rahisi wanaporudishiwa mipira na kupiga pasi ndefu au fupi na iwafikie wachezaji wao ili kuanzisha shambulizi. Hapa naamanisha, Diara akirudishiwa mpira na beki anahakikisha anapiga pasi inayofika kwa wachezaji wake iwe pasi fupi au ndefu. Diara habutui tu ilimradi mpira uende mbele tu. Kubutua mpira bila mwelekeo inakuwa ni hamsini kwa hamsini kule unapotua.
Jana tuliona golikipa wa JKT alipiga pasi ikadondokea kwa adui na mwisho wa siku ikazalisha faulo. Huyu kipa hana mazoezi ya kucheza mipira mirefu na mifupi kwa miguu.
2. Panchingi kwa mikono
Magolikipa lazima wajifunze wanapopanchi mipira iwe inaenda mbali ili hata kama inamfikia adui isiwe rahisi kushambulia kwa haraka. Hapa lazima mikono iwe na nguvu na wakipanchi wahakikishe mipira inaenda kwa juu tena pembeni.
Jana tuliona Diara alipanchi ila kwa kutoa pasi ambapo panchi ile ilienda pembeni kwa beki ya kushoto na shambulizi likaendelea, lakini golikipa wa JKT alipanchi shuti la Max na kumrudishia Max ndani ya uwanja. Diara asingepanchi vile kabisa.
Yote kwa yote, nilichokiona Diara yupo makini sana uwanjani. Macho yake na akili yake vinafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, hivyo inakuwa rahisi kucheza mipira inayoelekezwa golini, ndio maana Diara hata kama anafungwa lakini lazima mpira aufuate. Ni nadra sana Diara aende kulia, goli lipite kushoto.
Nawasilisha.