Magoma na Mwaipopo waangukia pua kesi dhidi ya Yanga

Magoma na Mwaipopo waangukia pua kesi dhidi ya Yanga

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Juma Ally Magoma na mwenzake Geofrey Mwaipopo waliyokuwa wameikata dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Dar es Salaam, Young African Sports, maarufu kama Yanga.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Septemba 9, 2024 na Naibu wa Mahakama hiyo, Livini Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi, Salma Maghimbi aliyeisikiliza rufaa hiyo.

Magoma na Mwaipopo walikata rufaa hiyo mahakamani hapo wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu kuiongezea Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga na wenzake muda wa kufungua shauri la maombi ya marejeo.
1725885871039.png
Yanga iliomba kuongezewa muda huo ili kufungua shauri hilo la marejeo ya hukumu ya mahakama hiyo iliyobatilisha Katiba yake ya sasa kufuatia kesi ya msingi iliyofunguliwa na Magoma na mwenzake, wakihoji uhalali wa katiba hiyo.

Soma Pia => Mzee Magoma Akata Rufaa, asema bado hautambui Uongozi

Wajibu rufaa katika rufaa hiyo walikuwa ni Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga (mjibu rufaa wa kwanza), Fatma Abeid Karume (mjumbe wa bodi hiyo mpaka sasa), Abeid Abeid na Jabiri Katundu, ambao pia waliwahi kuwa wajumbe wa bodi ya klabu hiyo.

Bodi ya wadhamini wa Yanga imewawekea pingamizi la hoja za kisheria kina Magoma dhidi ya rufaa hiyo, ikibainisha hoja mbili. Kwanza inadai kuwa uamuzi ambao kina Magoma wameukatia rufaa na ya pili wanadai kuwa rufaa hiyo imeshapitwa na tukio.

Pingamizi hilo lilisikilizwa Agosti 30 mwaka huu, ambapo mawakili pande zote Kalaghe Rashid wa Yanga na Jacob Mashenene wa kina Magoma walichuana kwa hoja za kisheria kila mmoja akijitahidi kuishaiwishi mahakama ikubaliane nao na kurejea kesi mbalimbali kusisitiza hoja zao.

Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake imetupilia mbali rufaa hiyo baada ya kukubaliana na pingamizi la Yanga kuwa uamuzi waliokuwa wanaukatia rufaa haukuapaswa kukatiwa rufaa kwa mujibu wa Sheria.

Credit: Mwanaspoti

Soma Pia =>
Juma Ally Magoma ameuonya Uongozi wa Yanga kuingilia kesi yake dhidi ya bodi ya wadhamini
 
Baada ya kesi ya muda mrefu kutoka kwa Mzee magoma na wenzake Godfrey Mwaipopo baada ya kukata Rufaa kwenye mahakama kuu Masjala Jijini Dar Es Salaam imekataliwa dhidi ya Bodi ya wadhamini wa klabu ya Yanga African Sports.

Magoma pamoja Mwaipopo kwa pamoja walikata Rufaa mahakamani wakipinga uamuzi wa Makamu ya Hakimu mkazi Mkoa wa Dar Es Salaam kisutu huku ikiongezewa Bodi ya wadhamini klabu ya Yanga muda wa kufungua shauri na marejeo.

Uamuzi umetolewa leo Septemba 9,2024 kutoka kwa Nahibu Mahakama hiyo, Livini Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi, Salma maghimbi ambaye ndio ameisikiliza rufaa hiyo.

Rufaa hiyo ilikuwa na wajibu kutoka Bodi ya wadhamini ya klabu ya Yanga ambaye alikuwa mjibu rufaa wa Kwanza Fatma Abeid karume ambaye ni mjumbe wa Bodi hiyo mpaka sasa, Abeid Abeid na Jabiri katundu ambao pia walishawahi kuwa wajumbe wa Bodi ya klabu ya Yanga SC.

Nahisi makolo wanawadanganya hawa wazee
 
Eng. Hersi aache woga. Akae meza moja na Mzee Magoma wayamalize kiume
Kwanini mzee Magoma hakukaa nao mwanzo akakimbilia mahakamani yeye? Kati ya Yanga na Mzee Magoma nani alifingua kesi mahakamani? Yanga wanapita na biti lake mwenyewe huyo mzee mjinga
 
Huyo kizee akipewa awanyweshe chai wachezaji anaweza kweli lengo lake haswa ni lipi? Au alikuwa na kamradi kake na hivyo kamefinyangwa?
 
Uyo mzee inavyoonekana alizoea kuwatikisa viongozi wa miaka Ile na alipokuwa anawatikisa walikuwa wanamuita wanampa vijisenti anachapa mwendo, sasa amezoea amedhani yanga Ile ndio hii ya sasa, kayakanyaga na viongozi wa yanga wanataka wakomeshe hii tabia isije kujirudia Tena kwa vizee kama hivi,
Alidhani Engineer atamwita ampe vijisenti yeye na mwenzake mwaipopo ili waupate angalau ela ya kula but kakutana na kitu kizito na ataishia pabaya na wanaomfadhili!
 
Ukiamua kutulia umsikilize kwa utulivu hoja zake, unaweza ukajihisi either umevutishwa bangi au unga au umepiga bapa za kutosha.
Anasema yeye ameslishitaki baraza la wadhamini la mwaka 1968 kwa katiba ya mwaka 1968, hawa wa sasa hivi wametoka wapi hadi waende kumpinga mahakamani
Yeye aliwashtaki FIFA au aliwashtaki mahakamani?
 
Back
Top Bottom