vivaforever
Senior Member
- May 30, 2016
- 113
- 165
1.Hutchson Gilford Progeria
Ni ugonjwa adimu zaidi ambao uwezekano wake wa kutokea ni kwa mtu mmoja miongoni mwa million 8 waliozaliwa. Huu ugojwa ni wa vinasaba(genetic) na mgonjwa wake huwa anazeeka haraka sana kuliko kawaida. Kiasi cha miaka anayoweza kuishi mtu mwenye Progeria kinakadiriwa kuwa ni miaka 12 hadi 15 ingawa kuna waliowahi kuishi hadi miaka 18. Mbaya zaidi huu ugonjwa hauna kinga wala Tiba.
2.Werewolf Syndrome
Huu ugonjwa unajulikana zaidi kama Hypertrichosis. Mgojwa mwenye ugonjwa huu huwa anaota nywele nyingi kupindukia kiasi cha kufanana na Wanyama pori kama Sokwe au Nyani. Baadhi huwa na nywele mwili mzima (generalized) huku wengine wakina na nywele kwenye baadhi ya maeneo tuu (Localized). Huu ugonjwa hauna kinga wala tiba ingawa kupunguza nywele za ziada kunasaidia ila hali hurudi tena baada ya siku hadi wiki kadhaa.
3. Proteus Syndrome
Pia hujulikana kama Wiedemann syndrome au Elephant man syndrome. Huu ugonjwa unamfanya mtu ngozi yake iwe nzito na kukua kupita kiasi. Mtu wa aina hii huwa pia na mifupa mizito pamoja na muonekano usio wa kawaida. Kundi la Madaktari Canada limegundua dawa ambayo inaelezwa kuwa ni chaguo sahihi la kutibu Proteus syndrome.
4.Fibrodysplasia Ossificans Progressiva (FOP)
Pia hujulikana kama Stone Man Syndrome, huu ugonjwa ni adimu lakini mbaya sana (badass). Mtu aliyeathirika na FOP misuli yake pamoja na Elastic tishu nyingine za mwili hubadilika na kuwa ngumu (hugeuka kuwa mifupa). Hakuna tiba wala kinga ya huu ugonjwa pia Upasuaji hufanya hali iwe mbaya zaidi. Sad.. 😢
5.Epidermodysplasia Verruciformis.
Kama kawaida yake huu ugojwa a.k.a yake ni Tree Man Syndrome. Moja kati ya magonjwa adimu zaidi duniani ya kivinasaba, mtu mwenye ugonjwa huu huota wagamba magumu mwilini mwake hasa usoni, vidoleni(mikononi na miguuni), Masikioni nk. Magamba hayo hukua haraka na kumpa ntu muonekano wa Mti. Mbaya zaidi hakuna tiba ya uhakika ingawa kuna mgonjwa mmoja walimtibu kwa kukata hayo mabaka lakino uwezekano wa kuota tena ni >90%
6.Cotard's Delusion.
Pia huitwa Walking Corpse Sydrome.Ni ugonjwa adimu sana wa kiakili ambapo mtu aliyeathirika huwa anaamini kwamba yeye ni mfu, huku wengine wakiamini kwamba wao ni Wamilele(Immortal). Wagonjwa hawa muda mwingi hukaa Makaburini wakiamini kwamba huko ndipo makazi yao yalipo. Tiba yake ni Madawa, Hemodialysis pamoja na Elimu ya akili.
7.Alien Hand Syndrome.
Alien ni kitu kigeni, ugonjwa huu huathiri neva za mtu hasa za mkononi na kuufanya mkono wa mtu ujongee(move) hovyo au kufanya utakavyo bila ridhaa ya mtu(involuntarly). Alien Hand Syndrome inaweza kuzuiliwa kupitia mazoezi hasa ya kushika vitu kwa kutumia mkono ulio athirika ingawa kinga haijulikani...
8.Aqua allergy
Aqua maana yake ni -ya kuhusihana na maji, huu ugonjwa ni adimu sana lakini ni mbaya kuliko ufikiriavyo. Mtu mwenye ugonjwa huu huwa anaumwa hapohapo akigusana au akinywa maji. Kiufupi ni ugonjwa unaotokea kama mtu akicome into contact na maji au kitu chochote chenye maji. Allergy ni Mzio kwa kiswahili, ugonjwa huu hauna kinga wala tiba... So bad!!
9.Exploding Head Syndrome.
Fikiria unajaribu kulala ghafla unasikia sauti kubwa kichwani mwako kama vile Bomu limeripuka, au watu wanapiga risasi, au Subwoofer limefunguliwa sauti kubwa, au aina nyingine yeyote ya kelele kubwa unapotaka kulala!! Hivyo ndivyo exploding head syndrome ilivyo.. Hupati dalili yoyote ya maumivu wala kizunguzungu hata vipimo kama Brain CT scan, MRI scan, Cerebral Angiography vitatoka vikowa clear kabisa (bila tatizo). Huu ugonjwa huwakumba zaidi watu zaidi ya miaka 50 ingawa hata watoto zaidi ya miaka 10 huwapata pia. Hamna kinga wala tiba..
10.Amyotrophic Lateral Sclerosis (ALS)
Pia ukijulikana kama Motor Neurone Disease au Lou Gehrig's Disease ni ugonjwa adimu ambao unasababisha seli neva za mwili zinazodhibiti matendo ya hiari kufa. Mtu mwenye ugonjwa huu huwa anaparalyse, misuli huwa migumu na inajipinda.. Ugonjwa huu ndio uliosababisha kifo cha Stephen Hawking. Sababu ya ugonjwa huu haijulikani kwa wengi ingawa wachache wameurithi. Dawa za kutibu ni kama vile Riluzole na Edaravone, dawa hizi hazitibu moja kwa moja bali hupunguza makali ya ugonjwa tuu.
Karibuni. 😊😊