Babu Swahili
Member
- Jan 8, 2009
- 41
- 6
Wenyeji wenzangu, nilikuwa na maswali machache kuhusu magonjwa haya ya zinaa
1) Kuna tofauti gani kati ya gonorea, kaswende, na kisonono.
2) Kaswende na kisonono yanaitwaje kwa kiingereza?
3) Human Papillomavirus (HPV) infection inaitwaje kwa kiswahili?
Mujaaliwe
1) gonorea ni sawa na kisonono kinaambukizwa na bacteria aina ya gonococcus wakati kaswende inaambukizwa na aina ya treponema. gono - inaanza kuonyesha dalili mapema kuliko kaswende na kaswende yaweza kwenda muda mrefu bila kugundulika - ambapo yaweza kuathiri mpaka ubongo.
2) kaswende ni syphilis wakati kisonono ni gonorrhea
3) sijawahi kusikia kiswahili cha HPV, tusubiri wataalam waseme zaidi.
wakuu pia kuna huu ugonjwa unaitwa LEPROSY,hivi kwa kiswahili unaitwaje?