Funuki Nungula
Member
- Jan 12, 2021
- 9
- 9
Duniani yapo magonjwa mengi sana ambayo yalitokea na kupotea na mengine bado yanaendelea. Na magonjwa mengine yanatisha watu wa rika zote na watu wa vyeo mbalimbali. Lakini Mimi napenda kukufahamisha magonjwa kumi(10) ambayo wanasayansi na madaktari bingwa hawajakuambia kuwa yapo na yanauwa Kama bila kubakiza kitu.
1. Kufikiri kuwa mtu mzima(mzazi) hakosei:- ugonjwa huu umeuwa familia nyingi mno, kwa sababu wazazi wengi eamewachokoza watoto wao na kubaki bila kuwaomba msamaha. Kwa hiyo mzazi mwenye mtazamo chana na familia yake lazima ajikinge na ugonjwa huu hatari.
2. Kuamini kuwa kuwa na elimu ya juu ni kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua changamoto:- wasomi wengi wa Karne hii wamefikia hatua yakuamini Kila jambo wanalofanya au kupanga ni sahihi kwa kuangalia viwango vyao vya elimu. Shida ni kwamba wamesahau kuwa wapo watu ambao viwango vyao vya elimu ni vya chini kabisa lakini fikra zao ni yakinifu na ni matunda mazuri ya baadaye.
3. Kuamini kuwa Kila anayekupa msaada anakupenda:- wapo watu wanaamini kuwa Kila anayekupa msaada anakupenda, la hasha!. Wapo watakao kupa msaada lengo lao ni kukusogeza ili wakufanye uwe karibu nao Kisha wakuuwe kiuchumi na kimwili kwa ujumla. Hivyo kuwa makini na ugonjwa huu hatari na wakutisha.
4. Kuamini kuwa Kila anayetangaza amani ni mtaka amani:- Kuna mataifa mbalimbali ambayo viongozi wake hupenda kutangaza habari za kutaka amani katika taifa, huku wao wakiwa mstari wa mbele kuchafua na kuvuruga amani iliyopo. Pengine ni watu tunao katika jamii zetu wanapenda kuongea habari za kuwa na amani, kumbe wao ndio wezi, wapolaji, majambaji na mafisadi wakubwa. Huu nao ni ugonjwa hatari jiepushe nao.
5. Kuamini kuwa kuwa tajiri ni kuwa adui wa Mungu:- wahubiri na wachungaji baadhi wamewafanya waumini wao kuwa maskini wa kutupwa kwa sababu ya kuwaaminisha kuwa matajiri ni adui wa Mungu. Huenda hawasomi vizuri biblia na kujua mkutadha wa baadhi ya maneno katika biblia. Iko hivi Mungu anahitaji watu wake waishi maisha mazuri wangali duniani. Ndio maana Amina Ibrahim, Sulemani, Ayubu na Daudi walikuwa matajiri. Fikra za namna hii ni mbovu na zinaua familia hadi taifa kwa ujumla.
6. Kuamini kuwa kuwa mcha Mungu ni kuwa adui wa watu:- waumini wengi wamekosa marafiki, ndugu, na hata jamaa zao kwa kudai wameokoka na kujikuta mambo yao yameyumba. Hili ni kushindwa kuelewa kuwa wajumbe wa kweli ya Mungu walisisitiza kuwa na amani na watu wote na hata Yesu mwenyewe wakati anawaombea wanafunzi wake, hakuomba wajitenge katika dunia bali walindwe na hila za shetani, soma kitabu cha Yohana sura ya 17 utaelewa na sio kuwa adui wa jamii yako.
7. Maisha mazuri huja kwa kuajiriwa:- hapo ndipo palipo na shida hasa kwa vijana. Wamejikuta wako palepale kiuchumi kwa kudai hakuna ajira huu ni ugonjwa wa akili na ni ukichaa na huenda usipotibiwa mapema utawapeleka vijana pabaya Sana. Hivyo Tiba yake ni kuchakalika na kuachana na mtindo wa kutembea na bahasha ya vyeti ukitafuta kazi.
8. Kuamini kuwa Watu pekee wabunifu na wataalamu ni wazungu:- huu nao ni ugonjwa hatari wa akili. Afrika ni bara lenye wabunifu wengi na vitu vyao wamekuwa wakivionyesha lakini havisapotiwi kwa kudhani ni feki kwa kuwa ni Cha mwafrika. Ni utumwa wa kifikra kabisa.
9. Kudhani kuwa kuwa kiongozi ni kuwazidi wengine uwezo wa akili hivyo huna haja ya ushauri kutoka kwao:- mataifa mengi yameyumba kiuchumi kwa sababu ya kuwa na viongozi wenye kujiamini binafsi, na kudharau maoni na ushauri kutoka kwa watu wengine wenye hekima zao. Kwa hiyo viongozi epukeni ugonjwa huu utawamaliza.
10. Kuamini kuwa mwanaume hapaswi kuomba msamaha kwa mke wake au mwenzi wake:- ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya dai Kama hilo. Jambo la kuomba msamaha kwa wenye ndoa ni la Kila mmoja. Ukiwa na fkra potovu Kama hiyo ugonjwa huo utaua familia yako.
Hayo ndiyo magonjwa hatari kuliko yote duniani na yapo na yanauwa taratibu lakini kwa uhakika.

Upvote
2