Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Kutokana na kalenda ya maradhi iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Oktoba ni maalumu kwa ajili ya kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti. Nikiwa daktari, binafsi naupenda mwezi huu kwa sababu unanipa fursa zaidi ya kuelimisha zaidi wagonjwa kuhusu aina hii ya saratani inayoongoza kutishia uhai wa wanawake kuliko aina nyingine zote.
Kisayansi, mwili unahitaji kiasi fulani cha seli zinazotengenezwa kutoka sehemu ya ndani ya mifupa. Seli hizo ni muhimu kwa afya na uhai, lakini kama zitazalishwa kwa kiwango kinachoweza kuhimili mwilini.
Wakati mwingine seli hizo huzalishwa zaidi ya kiwango kinachoweza kuzimudu, hivyo kusababisha kujikusanya na kujiweka sehemu moja na kutengeneza uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Ikitokea seli hizi zinajikusanya kwenye moja ya tishu za titi na kutengeneza uvimbe, hapo ndipo saratani ya titi inapoanza.
Takwimu zinaonyesha zaidi ya wanawake milioni 7.1 wanagundundulika na saratani hiyo kila mwaka dunia. Saratani ya matiti imekua tishio kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwamo na sababu kubwa ni kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.
Ili kuepuka maradhi hayom ni kwa wanawake kupima mara kwa mara ili kuiwahi ikiwa katikahatua ya awali. Kama ilivyo kwa saratani za aina nyingine, jambo pekee muhimu linaloweza kuokoa maisha ya mgonjwa wa saratani ya matiti ni kuwahi kufanya vipimo. Kwani inatibika ikigundulika ikiwa katika hatua za awali.
Wanawake wengi hupoteza maisha kwa ugonjwa huo kwa sababu huenda kupata vipimo wakati ameugua kwa muda mrefu.
Kitu kingine muhimu cha muhimu ni kuzitambua dalili za awali. Wanawake wanashauriwa mara aonapo dalili ni vema akawahi vipimo na matibabu.
Miongoni mwa dalili za ugonjwa huo ni maumivu chini ya kwapa na kwenye matiti yanayotokea mara kwa mara, rangi ya ngozi ya titi kubadilika mara kwa mara na kuwa aidha nyekundu au kama rangi ya chungwa, muonekano wa chuchu kubadilika, kutoa kimiminika chenye mchanganyiko wa damu.
Pia, mabadiliko ya kimaumbile na ukubwa wa titi na dalili nyingine kuu ni kuhisi uvimbe mgumu unaoanza kujitokeza kweye titi moja na mara nyingi uvimbe huo hautoi maumivu. Japo kuwa si kila uvime kwenye titi unaashiria saratani, ni vema kujenga utamaduni wa kupima mara kwa mara, hasa unapohisi una uvimbe kwenye titi.
Wanawake pia wanapaswa kufahamu namna ya kukabiliana na saratani ya titi na mazingira yake hatarishi ya kupata ugonjwa huu.
Zipo sabababu nyingi zinazomuweka mwanamke kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.
Japo kuna baadhi ya sababu ni vigumu kuziepuka, lakini ni vema kuzitambua ili zile zinazoepukika, mwanamke ajiepushe nazo.
Sababu ya kwanza ni umri. Mwanamke anakua hatarini kupata saratani hiyo kadiri umri unavyojongea.
Uwezekano wa kupata saratani ya titi unaanza mtu akiwa na miaka 20 hadi 30. Uwezekano huu unadumu hadi kwenye miaka 70. Hivyo, ni vema kujenga utamaduni wa kupima mara kwa mara ukiwa na miaka 20 hadi 70.
Sababu za kurithi pia zinachangia uwezekano wa kupata saratani hiyo ya titi. Japo si mara nyingi, lakini wakati mwingine mwanamke anaweza akawa na vinasaba vinavyosababisha ugonjwa huo wa saratani ya titi. Vinasaba hivi kisayansi vinaitwa BRCA. Hivyo, ni vema kujua historia ya ukoo wako na kupata vipimo ili ujue kama una vinasaba hivyo.
Kwani kwa kufanya hivyo, unajiweka katika hatua nzuri ya kuepukana na saratani ya titi itokananayo na sababu za kurithi.