SoC01 Magonjwa ya Afya ya akili yanatibika, vunja ukimya

Stories of Change - 2021 Competition

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
20,178
Reaction score
39,641
" Daktari huwezi kuelewa ntakachokuambia bora nife nacho " yalikua ni maneno ya mgonjwa wangu niliyekua namhudumia kwa muda mrefu , niligundua ana matatizo zaidi yanayopelekea afya yake kudhorota siku baada ya siku

Afya ya akili kwa kimombo (mental health) ni swala ambalo limekua likichukuliwa kwa mzaha katika jamii zetu za kiafrika , ukisikia kuhusu afya ya akili ndugu msomaji akili yako lazima itakupeleka moja kwa moja kuwaza " UKICHAA " .

Afya ya akili sio ukichaa , afya ya akili ni uwezo wa akili mtu kufanya vitu kwa usahihi , kufikiri kwa usahihi , kutenda kwa usahihi , Ni uwezo wa ubongo kuchanganua mambo na kuyafanya kwa usahihi, mtu unaweza usiwe kichaa lakini hutendi kwa usahihi au hufikiri kwa usahihi . Unawaza kufa tu kila saa unawaza dunia yote imekutenga hayo yanaweza kuwa ni mawazo yako lakini sio sahihi

Ubongo wa binadamu umetengenezwa kwa namna ya tofauti sana tatizo lolote linaloweza kutokea kwenye ubongo linaweza kupelekea matatizo mengine mengi kwenye viungo vingine vya mwili unachukua asilimia mbili tu ya uzito wa mwili mzima lakini asilimia ishirini ya nishati nzima ya mwili inapelekwa kwenye ubongo, wanasayansi bado tunajaribu kuchunguza uhusiano wa matatizo ya akili na reaction mbali mbali zinazotokea kwenye ubongo lakini kwa uchache (nitatumia lugha rahisi ili kila mtu hata asiyesoma sayansi afahamu) naweza kusema matatizo mengi ya afya ya akili yanatokana na kukosekana kwa uwiano katika kemikali mbalimbali za saketi kwenye ubongo (neurones) mfano wa kemikali hizo ni serotonini na neuroepinephrine (nimekosa neno lake la kiswahili ).

Hizi nyuroni huwasiliana zenyewe kwa zenyewe na katika kuwasiliana hutumia kemikali nilizozitaja hapo juu na zingine nyingi inapotokea hakuna uwiano wa kemikali ndipo hapo mtu tunasema ubongo wake umepata shida na hafanyi mambo kwa usahihi mfano kunapokua na utengenezwaji mwingi wa kemikali ya dopimine katika saketi za ubongo hapo ndipo tunasema mtu ana ukichaa uliopitiliza( psychosis) , ndo hawa tunawaona wanaokota makopo kwenye mabarabara.

Kwa mtu mwenye msongo mkubwa wa mawazo inamaanisha kemikali za serotonini zinatengenezwa kwa kiwango kichache sana katika nyuroni zake za ubongo , serotonini sisi wataalamu wa afya hupenda kuiita " kemikali ya furaha" sababu ikipungua furaha ya mtu hupungua na hata hamu ya kula hupungua.

Kwa hiyo ubongo ni kama kiungo chochote kila kwenye mwili kwamba na chenyewe kinaweza kuumwa na kinaweza pata ajali hata maneno tu yanaweza kufanya ubongo upate ajali mfano unatukanwa au unadhalilishwa na mtu unayempenda kila siku na shida kubwa inakuja kwamba ubongo ndo unaongoza ogani zingine za mwili hivyo unapopata shida ogani zingine zitadhurika pia na hilo ndilo lilikua linatokea kwa mgonjwa wangu nliyemtaja mwanzo wa hili andiko

kwa hiyo kama tulivyoona hapo juu kwa uchache afya ya akili ni jambo linalohusu kukosekana kwa uhusiano wa kemikali mbali mbali za ubongo ,Hivyo jamii inapaswa itambue kwamba ukiwa na tatizo la akili sio kwamba wewe ni kichaa ni kwamba umeumwa kama unavyoweza kuumwa meno au mguu ndio ukichaa ni ugonjwa wa akili lakini sio kila ugonjwa wa akili ni ukichaa , sisi kama jamii inapaswa tuwe na uelewa wa kuweza kuwsaidia watu mbali mbali wanaopitia matatizo ya afya ya akili wakiwemo vichaa bila kuwabagua.

Mtu anapokufuatwa na kukuelekeza shida yake jaribu kumsikiliza kama vile tulivyoona kwamba maneno yanaeza kuuletea ubongo ajali tafiti zinaonyesha maneno ya kufariji na kutia moyo yanaweza kupelekea mtu akapata ahueni katika mambo yanamkabili . Mtu akikwambia ana msongo wa mawazo tusimuone kama mtu weak mtu anayejiendekeza hii ipo kwetu sana wanaume na ndio wahanga wakubwa wa magonjwa ya akili.

Usikimbilie katika kufanya hitimisho la nini anaumwa msikilize kwa umakini , tafuta sehemu iliyotulia ongea nae sio lazima ukubaliane na anachoongea lakini kwa kuonyesha unajali hisia zake utakua umemsaidia pakubwa sana , muulize maswali machache yanayoweza kumfanya aongee zaidi lakini sio maswali yanayoweza kumfanya ajihukumu zaidi

Tunakutegemea wewe unayesoma hapa kuwa nyenzo ya kutuletea mtu mwenye magonjwa ya akili ili sisi tushughulike nae kitaalamu zaidi , jaribu kumshauri kwamba inapaswa awaone pia wataalamu wa afya hapo ni baada ya kumshauri maneno kadhaa ya kutia moyo na kubwa katika yote angalia na umsome huyo mtu kama ana mawazo ya kujidhuru na u deal na hilo jambo haraka kadri unavyoweza

katika makala zingine zinazofuata tutaongelea nini mtu anapaswa kufanya anapohisi ana tatizo la afya ya akili , hatua za kuchukua na pia tutaongelea nini serikali inapaswa ifanye kutatua matatizo haya leo tumeongelea jamii inapaswa ifanye nini na ielewe nini kuhusu afya ya akili usisahau ku vote kwenye alama ya ^ hapo chini

NIMALIZIE KWA KUSEMA " MAGONJWA YA AKILI YANATIBIKA VUNJA UKIMYA"
Asanteni sana
 
Upvote 98
Usahihi ni Upi ?

Tusije kuona Utofauti ndio Usahihi ?. By the Way mwenye Ugonjwa wa Akili anajitambua na kujisema kwamba hayupo Sawa ?

Anyway nadhani binadamu wote tuna ka-disjunction kidogo upstairs, cha maana sio kunyanyapaa watu wala kulazimisha watu kwamba wanahitaji msaada (ili wawe kama sisi) ila kama wakija kuomba msaada hatuna budi kuwapa...
 
Pamoja sana mkuu

Una swali lolote

nGoja nitoe maelezo kisha ndio swali lifuate , Kuna member humu awali alikuwa mwanasiasa na mwalimu na alikuwa bright tu ,sijui kitu gani kimempata akaanza kuandika matusi na mambo yasiyoeleweka facebook ,akakamatwa na kufungwa baadae akatoka ,lakini ukimcheck mambo anayofanya ni kama mtu ambaye dish limecheza(ana matatizo ya afya ya akili) ,cha kushangaza anaingia kwenye mitandao fresh na kupost kazi zake za muziki ambayo ukisikiliza unaona kabisa hayuko sawa.

Swali langu hivi mtu kama huyo tunaweza kumuweka kundi gani? Maana haakoti makopo ila mambo anayofanya awali na sasa unaona jamaa hayupo sawa kichwani lakini anaongea na kucomment vizuri kwa swali aliloulizwa.

Je anaweza akatibika?
 
Mtu mwenye ugonjwa wa akili anaweza akawa na ugonjwa wa akili na asitambue akajiona yupo sawa hiii ni kwasababu
Hafahamu chochote kuhusu ugonjwa wa akili

Lakini pia anaweza asifahamu kuhusu ugonjwa wake kwa sababu ubongo umeharbika kiasi cha kutojua lipi ni sahihi na lipi sio sahihi hata kama mwanzo ulikua unajua ni sahihi mfano mimi nikipata ukichaa sasa hivi " psychosis

mtu mwingine anaweza Pata ugonjwa wa akili na akatambua kuna vitu haviko sawa kama vile, kumbukumbu kupotea
Au kushindwa kutambua watu tena

Nimejaribu kukujibu
 
Okay nimekupata.....

Ingawa pia unaweza kukuta mtu yupo sawa (unique) ila kwa mtizamo wa jamii na kutaka kumbadilisha kama jamii inavyotaka mkajikuta kwamba mnampoteza...

Yaani kuondoa ile confidence yake katika utofauti wake... (mfano mtu anaweza akawa mchangamfu sana kama chizi, yaani a happy go lucky guy) ila jamii kumuona kwamba hafai au inabidi ku-behave in such a different way ukajikuta kwamba unambadilisha chui anakuwa paka....

My point is we are all different tusije tukafanya kosa la kutaka kuwaondoa watu wenye behaviour tofauti na sisi kwa kuwa-label mafyatu (There is nothing worse than questioning yourself, kweli ukifikia hapo utakuwa hauona tofauti na robot inayokuwa programmed kufanya kila watu wanataka) And that's not being a Human...
 
Namna gani huo ugonjwa unatibika!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitarudi kukuelekeza kwa undani unajua ubongo wetu umetengenezwa kufikiria vitu sahihi na vinavyoweza kukuletea mambo chanya kwenye maisha unapochukua muda mwingi kufikiri kitu ambacho hakina faida yeyote kwenye maisha yako ya kila siku kinachotokea ni kwamba afya yako ya akili inadhorota siku baada ya siku
Mara nyingi hizo impulsive thinking zinakua either tunafkiria mambo yaliyopita au tunafikiria mambo ya mbele yetu yatakuaje (hofu)

Siku zote kadri unavyojaribu kuyazuia mawazo flani ndo kama unachochea moto kwenye petroli kwa hiyo tunachofanya ni kujaribu kutengeneza chanell nyingine ya mawazo mfano unaweza tafuta activity mpya ya kufanya kama vile kujifunza kitu kipya hata kama yale mawazo yatakuja hayatakUa kama mwanzo na kubwa kuliko yote ni kujisamehe.... Ntarudi
 
Upo sshihi kabisa mkuu tuna aina tofauti kabisa za personality mfano mimi nshawahi kuwa na mdada ni narcissist aloooh πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸšΆ
 
Itakuwaje endapo mbinu hiyo ikagonga mwamba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aah unamuongelea nanii.... πŸ˜‚

Sasa mkuu muda mwingine magonjwa ya akili yanatokana na matumizi yaliyopitiliza ya mihadarati sitaki kusema yeye ametumia mihadarati kupitiliza hapana
Mihadarati mfano cannabis au lsd humpa mtu hali ya kujiamini kupitiliza kuweza hata kuitukana serikali unaweza enda hata mbele ya psu pale ukawambia hamna cha kunifanya nyie na ndo tunachokiona kwa jamaa lakini pia mtu akiwa na stress za muda mrefu mrefu sana anaweza pata hali ya severe mental illness kama jamaa
Pia inaweza ikawa urithi, ukichaa, schizophrenia muda mwingine ni genetically inherited

Ntakupa story ya mwanasayansi mmoja marekani anaitwa John nash huyu jamaa alkua na schizophrenia lakini na matatizo yake ya akili aliweza kutengeneza vitu kama vile game theory, differential geometry, na study of partial differential equations jamaa na matatizo yake yote alileta mabadiliko makubwa kwenye nyanja ya uchumi na akashinda nobel prize mwaka 94 pia kwenye saikolojia ana mchango wake kwa hiyo point yangu mtu anaweza akawa ana mental illness na akawa anafanya vitu vingine fresh tu anaweza akapona akipata matibabu au madhara yakapungua

Nimejaribu kukueleza... Swali lingine mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…