Magonjwa ya Nguruwe

pasodz

Member
Joined
Jan 19, 2015
Posts
59
Reaction score
10
samahan wanajamv naomba kujuzwa juu ya magonjwa yanayoweza kumkabir mnyama aitwaye nguruwe maana nataka nifuge ili nipate mtaji natanguliz shkuran
 
Ukiacha magonjwa ya mlipuko,kama swain fever,nguruwe ugonjwa wake mkubwa ni minyoo.Mpe dawa za minyoo kila baada ya miezi 3 kama chakula ni pumba na mashudu ila kama ni mabaki ya chakula cha binadam mpe dawa kila baada ya miezi 2.
 
ushauri uliotangulia mzuri kwer ni minyoo kweri na wakati mwingine manyoya unyauka kwa ilo wapake oil chafu kuuwa wadudu na dawa za minyoo waweza kuzidunga au vidonge kuvisaga na kumix kwenye pumba na mlo mzur ni pumba iliyochanganywa na damu kavu na maji ya kunywa
 

nashkuru aisee!
 
Changamoto kubwa na za kawaida kwa nguruwe ni kama ifuatavyo :-
Kwa vitoto_ upungufu wa damu (wachome iron dextran), kuhara (imarisha usafi, wachome sulphur drug) na homa ya mapafu yaani pneumonia (epuka ubaridi wa sakafu, wachome antibiotic hata OTC).

Wakubwa, hawa kushambuliwa na magonjwa sio sana, ila tatizo lao kubwa ni kushambuliwa na vinyonyaji (parasites) hasa minyoo na utitiri unaopelekea ukurutu na kujikuna (wape dawa za minyoo kila baada ya miezi mitatu na dawa za utitiri, imarisha usafi wa banda). Lishe bora ni muhimu sana. Matatizo mengine yanasababishwa na lishe duni, abnormal metabolism, ajali mbali mbali n.k....
Karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…