Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yatatumaliza. Tuamke

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yatatumaliza. Tuamke

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Kwa mujibu wa ripoti ya WHO, magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua Zaidi ya watu milioni 41 kila mwaka, hii ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote vinavyotokea duniani.

Magojwa ya moyo na mfumo wa damu ndiyo huongoza kwa kusababisha vifo ikifuatiwa na saratani, magonjwa ya mfumo wa fahamu Pamoja na kisukari.

Tumekuwa tunapiga kelele sana kuhusu magonjwa ya kuambukiza ambayo mengi tumefaulu kuyajua kwa undani wake. Ni lini tutaanza kuzungumzia upande wa pili wa magonjwa yasiyo ambukizwa kabla hayajatumaliza?

Ugonjwa wa UVIKO 19 ulipozuka miaka ya hivi karibuni dunia nzima iliamka, ugonjwa wa homa ya nyani kadhalika. Hii ni mifano miwili tu kati ya mingi, kumbuka pia UKIMWI, polio, kisonono, kaswende n.k

Naelewa kuwa baadhi ya magonjwa hasa yale ya mlipuko hupaswa kushughulikiwa kwa uharaka na tahadhari kubwa ili yasilete maafa makubwa kwa jamii ndani ya kipindi kifupi. Hata hivyo, jambo hili halitoi uhalali wa kutokushughulikia magonjwa mengine.

Takwimu za magonjwa haya zinatisha, na zinazidi kuongezeka kila mwaka.Ni wakati sasa wa serikali, wadau, taasisi Pamoja na watu wote kwa umoja wetu tuanze kutoa kipaumbele kwa aina hii ya magonjwa ambayo huutafuna mwili wa binadamu na kuleta madhara mengi yenye mlengo hasi wa kufupisha uhai.

Tuamke sasa kabla hatujakwisha!
 
Kwa mujibu wa ripoti ya WHO, magonjwa yasiyo ya kuambukiza huua Zaidi ya watu milioni 41 kila mwaka, hii ni sawa na asilimia 71 ya vifo vyote vinavyotokea duniani...
Hili ni janga kwa kweli pamoja ya kuwa wanasema ni mtindo wa maisha ila haya mazao ya kisasa tunayotumia baada ya kukataa mazao ya asili tutapata taabu sana maana hamna mbadala wa mazao hayo
 
Back
Top Bottom